Welcome “karibu” to Tabora (Mboka or Kazeh) and to Uyui- by Maganga Feruzi

The map of Tabora Tanzania, Mboka or Kazeh (magangaferuzi@gmail.com)

Thanks for visiting this site and you will never regret.Welcome to this wonderful and informative site of Uyui. Uyui is at the heart of Tabora Region (Young Generations called it- MBOKA and Elderly they used to KAZEH) in the western part of the United Republic of Tanzania. Not many people are aware of its beauty and the compassionate of its people. The Wanyamwezi, a popular tribe whose people are lovely and full of aptical culture that is demonstrated by their simple life. Wanyamwezi are the local residents of Tabora.Karibu (welcome) to Uyui so that you can learn the untold story and the wonderful lifestyle of Wanyamezi Tribe (Wanyanyembe, Wakonongo, Wasumbwa etc).

Write to us magangaferuzi@gmail.com  tuandikie magangaferuzi@gmail.com

Kufungia Stori 1

Uyui: Dar cautioned on fore casted rains_Dar yatahadharishwa kuhusu ujio wa mvua kubwa

Dar residents have been cautioned to take precaution on the forthcoming heavy rains as fore casted by Meteorological Authority.

 

Wakazi wa Jiji la Dar es salaam na mikoa ya jirani wametadharishwa kuhusu uwezekano wa kutokea mvua hivyo wachukue tahadhari.

Uyui: Rest in Peace Our Dearest Aunt Mwajuma Saidi (Mama Nyamizi) of Chemchem

We are from Allah and to him we shall return.

This is all we can say and Praise the Lord for giving Us our dearest Aunt to have her wisdom and guidance for all these years.

Mwajuma Saidi (Mama Nyamizi) these were her names but we never called her any name rather than Shangazi or else Shangazi Mama Nyamizi.

The Late Mama Nyamizi is one of the Elders of Tabora, Chemchem Ward and Amani Street. A very polite and intelligent Old lady who carried in her shoulders all the responsibilities of guiding a very large families after her brothers passed away. She never showed any sign of giving up from those responsibilities. Despite our tears we are proud of her and pray to the almighty Allah to forgive her sin and put her to firdous.

The late mama Nyamizi will be laid to piece today at 4.00 pm in the evening. Dear Aunt, Inna Lilahi Waina Ilayhi Rajiuuun.

Uyui Day Celebrated on 29 July, 2017 (A re-Union after 30 Years of Uyui)

That was a day, a historic one at the Institute of Social Work, where all the memories down the lane were lively brought up. The colorful occasion was attended by old students of Uyui who studied at the school from 1970s to date, some coded themselves as Wahenga (Old wise man).

It was a re-union day where the old students of those days (now parents and Grand pa) who left one other had a chance to meet again. It happened after a period of 30 to 35 years of which by any definition was a long period.

To make the story short on how it happened, the social network (Whatsup platform) has helped the old students to re-unite and have the opportunity to cherish the old golden good days, make some light jokes, having funny, make some physical exercises, play football, having soft drinks and later to the dancing floor a favorite stuff that was enjoyed by almost everyone who attended.

A unique day had unique things, one of the memorable thing that happened was a name of their Head Master Mr. Kandubhai Patel (R.I.P), they all associated and labeled themselves as Patel’s son and daughters. (Watoto wa Mwalimu Patel). They were and still proud of their head master, Mwalimu Patel was a Wise Head master whose caring and helping hand had helped most of the students who studied at Uyui during his leadership. Mwalimu Patel remained a symbol of Uyui for the Old Students and every Old student has been proud to be associated with him. Uyui is about Mwalimu Patel and the two can not be separated.

Ooh let me go back to the story or let me organize it and bring it up with some photos if I will manage to have few. stay tuned.

Miaka 10 ya Soka la Tanzania Bila ya Said Mwamba Kizota (R.I.P- Said)

SAID NASSORO MWAMBA “KIZOTA”

Buriani Said Nassoro Mwamba “Kizota” mtambo wa magoli na Nyota ya Magharibi iliyozimika ghafla.

NI MIAKA 10 imepita sasa lakini nakumbuka ni kama tuliko lililotokea jana.  

ilikuwa tarehe 11 February, 2007 majira ya saa nne usiku nilipata ujumbe mfupi wa simu kutoka kwa Swedy Mwinyi wa Radio Tanzania, “.. salaam, Said Mwamba amefariki dunia kwa kugongwa na gari wakati anatoka Taifa!! Maiti ipo Mortuary Temeke..” Taarifa hii ya msiba, tena ya mtu unayemfahamu lazima imshitue mtu. Nilishituka sana baadaye nikamshukuru Mungu. Nilipigia simu mmoja wa Jamaa na rafiki wa karibu wa marehemu Said, Mchezaji wa zamani wa Simba na Yanga Kureish Ufunguo ambaye muda mfupi uliopita nilikuwa namtania kuhusu matokeo ya mechi ya Simba ya jana. Naye alishituka sana, masikini, naye  hakuwa na taarifa akaniambia labda tumuulize Isack Gamba wa Radio One, nilipompigia akasema ni kweli!!. Ndivyo yalivyo maisha ya mwanadamu hapa duniani, kama Ua huchanua na kusinyaa.

Kwa mtu yeyote aliyemfahamu marehemu Said, atakiri na kukubaliana nami kuwa Taifa limepoteza mmoja wa mashujaa wake aliyelipigania Taifa lake katika medani ya Soka enzi za uhai wake. Alikuwa na kipaji cha ajabu katika soka na aliufanya mpira jinsi alivyotaka yeye.

Marehemu Said Mwamba alizaliwa na kukulia mjini Tabora kabla ya kuja Dar es Salam miaka ya 1980 katikati ambapo baadaye alijiunga na  Dar es Salaam Youngs Africa (YANGA). Ameifanyia mengi Klabu hii ya Jangwani ambayo licha ya kuwa mchezaji alikuwa ni mdau wake mkubwa.

Kwa kipindi cha takribani miongo mitatu iliyopita Tabora ilikuwa ni mji uliotoa wachazaji wengi wenye vipaji tangia enzi za Gosaji Cup miaka ya 1960 kama Yunge mwana Sali, Hasan Rajab, Mzee kitenge na wengineo. Miaka ya 1970 kukawa na timu imara kama Sungura, Coastal, baadaye Tumbaku, Tindo, na Vita iliyokuwa Timu ya Jeshi enzi za Meja Jenerali mstaafu Mayunga alipokuwa mkuu wa Brigedi ya Magharibi.

Wakati marehemu Said anaanza kucheza mpira yeye na ndugu zake kina Rajabu na Ally Mwamba, kina Ufunguo na Abas Mchemba tayari Tabora imelishawahi kutoa wachezaji wenye vipaji walioliwakilisha Taifa kama kina Amasha, Athumani Maulidi-Big man, Hamis Kinye,  marehemu Athumani Mambosasa, Rajab Risasi, Abdallah Mwinyimkuu pele ambao walimsawishi marehemu Said kuongeza bidii.

walikuwepo pia watu waliosomea shule za Tabora kama Daudi Salum Bruce Lee na marehemu Ibrahim Marekano Regan ambao walipata mafanikio makubwa na kuchezea timu ya wekundu wa Msimbazi Simba ziku za nyuma. Tabora ilikuwa na kituo cha kuibua vipaji vya watoto wadogo cha kanisa katoliki Tabora kilichokuwa chini ya ulezi wa father Damiano cha Chipukizi.

Ndani ya uwanja marehemu Said alikuwa na uwezo wa kucheza karibu namba zote. Alipotoka Tabora na kujiunga Yanga alikuwa anacheza nafasi ya kiungo mkabaji. Baadaye waalimu kama sikosei ni marehemu Tarzan alimbadili na kumfanya acheze kama mshambuliaji wa kati.  Kuna wakati nilimuuliza sababu gani ilimfanya aende Simba kabla ya kuridi tena Yanga, akatabasamu na kuniambia kuwa mpira una mambo mengi.

Said alikuwa na uwezo mkubwa wa kupiga chenga tena za maudhi halafu anaukanyaga mpira na kuwaangalia wachezaji wa timu pinzani kama anayeuliza maswali? Kutokana na uwezo wake wa kumiliki mpira alifananishwa na jinsi marehemu baba wa Taifa alivyokuwa anaendesha vikao vya Chama kule kizota alipokuwa akiuliza maswali? Huku wajumbe wakisema hakunaa.

Wapenzi wa kandanda watakubaliana nami kuwa marehemu Said alikuwa na kipaji kikubwa. Mwaka 1993 alikuwa ni miongoni mwa wachezaji walioiwezesha  Yanga kuutwaa Ubingwa wa Afrika ya Mashariki. Enzi hizo walikuwapo kina keneth Mkapa, Nemes, Mohammed Hussein Mmachinga, Abubakar Salum, Mwanamtwa Kihwelo, Zamoyoni Mogella, Edbily Lunyamila, marehemu Steven Mussa, Gagarino, marehemu Method Mogella na marehemu Riffat Said.

Marehemu Said Mwamba, mbali ya mafanikio aliyopata ndani ya uwanja, nje ya uwanja aliuweka kando u-super star wake, hakuwa mtu wa kujidai, alikuwa hawezi kumpita mtu aliyemfahamu bila kusimama na kumsalimia. Kuna habari ambazo sikuwahi kumuuliza marehemu said kama kweli alishawahi kuukataa uraia wa moja ya nchi za kiarabu (Abudhabi) ili aendelee kuchezea Yanga.

Wapo wachezaji ambao hata wenzao wanawakubali. Said ni mmoja wa wachezaji ambao hata wa Timu ya Taifa mwaka 2000 wakati tunajiaanda kucheza na Ghana wachezaji wenzake walimtaka kocha mkuu wa timu ya Taifa Mjerumani Bukhard Pape awaite kikosini Kizota na Masatu ili achwe huru  kama wanamfaa

Nilipomuuliza kama kuna Timu nyingine aliyowahi kuipenda kama Yanga, marehemu Said alisema kuwa alikuwa anapenda sana uchezaji wa Timu ya Pamba wana kawe kamo enzi hizo ilipokuwa kwenye kiwango.

Taifa na wapenzi wa mpira hasa wa Yanga wamepata msiba mkubwa na vivyo hivyo kwa hata kwa wapenzi na wanachama wa Simba ambao marehemu alipata kuchezea.  Kwa hali yeyote iwayo msiba huu ni mkubwa sana Tabora kwa sababu mji huo umepoteza mmoja wa watoto wake wenye vipaji vikubwa iliyopata kuwazaa. Wapo wachezaji wengi lakini alikuwapo Said Mwamba kizota mmoja na pengine itachukuwa miongo kadhaa kumpata wa mithili yake.

Wapo wachezaji wengi lakini alikuwepo Said Mwamba Kizoto Mmoja tu Tanzania.Buriani Said Mwamba kizota umetangulia kule ambako sisi tuliobaki tutakufuta. Wote tumetoka kwa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.

Kuna mtu amewakumbuka aliomaliza nao darasa la 7 mwaka 1978 (Miaka 39 iliyopita)

CHEMCHEM SHULE YA MSINGIDarasa la saba Chemchem 1978 (Miaka 39 iliyopita)

INAWEZA isiwe habari kubwa lakini kuna mtu amekumbuka orodha ya wanafunzi wenzake aliomaliza nao darasa la 7 mwaka 1978, takribani miaka 39 imepita sasa. Kitu ambacho Uyui imevutiwa nacho ni uwezo wa kuwakumbuka watu hao ambao kwa sasa ni watu wazima na wengine watakuwa pengine wamekwisha tangulia mbele ya haki. Kwa atakaona jina lake ajue amekumbukwa na anaweza kutuletea simulizi au kisa au habari yoyote ya masomo na shule yao (sio lazima iwe Chemchem) nasi tutaichapisha kwa haraka kwa kadiri inavyowezekana. pengine inaweza ikawa re-union, nani anayejua? muwe na jumapili njema.  Poleni pia kama orodha hii itawaboa wengine

 1. Mashaka Hassan Rajabu
 2. Mwajumbe Hassan Rajabu
 3. Tamasha Iddi Ludete
 4. Sokolo Selemani Madema
 5. Ali Mohammed (Mangi)
 6. Tatu Mohammed (Mangi)
 7. Mgeni Athumani
 8. Jampani Venus
 9. Mohammedi Msulunguti
 10. Saidi Sudi
 11. Rajabu Risasi
 12. Makusudi Akili Tumbo
 13. Moshi Hassani
 14. Omari Hassan Kanonkola
 15. Seligei Mutahiwa
 16. Kulwa Shabani Mambo
 17. Matulanya (Gombo) Makoye
 18. Mussa Iddi (Fibrosi)
 19. Mussa Iddi (Totoro)
 20. Nassoro Msenda
 21. Veronika ……..
 22.  Nkulanga Gohima
 23. Mariam Seif
 24. Hazina Seif
 25. Titi Mussa
 26. Mussa Kiongozi
 27. Bakari Sembogo
 28. Noah Daniel
 29. Mohammed Hassan Kaombwe
 30. Hamis Mohammed
 31. Mwanaisha Ahmed
 32. Msabila Iddi
 33. Said Kassimu
 34. Amadi Selemani
 35. Desderi …..
 36. Mbaya Hamisi
 37. Sadi Kitwana
 38. Mkiwa Rashidi
 39. Zaituni Haji
 40. Ali Rashid
 41. Amina Mrisho
 42. Mosi Jumanne
 43. Rehani Malingo
 44. Hamisa Msafiri
 45. Katawanya Rashidi
 46. Hussen Salumu
 47. Kabichi Nasri

Orodha ya Walimu Chemchem shule ya Msingi 1971-1978 (waliofundisha nyakati mbalimbali)

 1.  Mwl. Iddi Chaurembo
 2. Mwl. Richard Guliku
 3. Mwl Aborgasti Mkangara
 4. Mwl Jaafar Mgumia
 5. Mwl Tatu Salmini
 6. Mwl Zainabu Iddi
 7. Mwl Mwenda (Lady)
 8. Mwl Luleka
 9. Mwl FakhI
 10. Mwl Sarah (alifundisha BTP mwaka 1975) alifundisha darasa la 4 masomo mengine ikiwemo sanaa
 11. Mwl Selemani Saidi (Alipenda kusema …”… ajabu ya Mungu..” na wanafunzi wakawa wanamuita hivyo hivyo
 12. Mwl Ester Abubakar Alawi
 13. Mwl Njau

 

Uyui: Magazeti ya Leo 4 February, 2017 (4th February, 2017 Newspapers- Front and Lead Stories)

Tanzania News Papers Round-up this Friday 3 February 2016 (Sura za Mbele za Magazeti ya leo)

Magazeti ya Leo  kwa hisani ya Michuzi Blog 

Form IV Results (2016) are Out. Matokeo ya Kidato cha IV yametoka

SHULE ZILIZOINGIA 10 BORA KITAIFA 2016 KIDATO CHA IV:
Feza Boys Sec School – Dar es Salaam
St. Francis Girls Sec School –Mbeya
Kaizirege Junior Sec School – Kagera
Marian Gilrs Sec School – Pwani
Marian Boys Sec School- Pwani
St. Aloysius Girls Sec School – Pwani
Shamsiye Boys Sec School – Dar es Salaam
Anuarite Girls Sec School- Kilimanjaro
Kifungilo Girls Sec School- Tanga
Thomas More Machrina Sec School – Dar es Salaam

bofya hapa kwa matokeo zaidi

http://41.188.136.77:8080/matokeo/2016/csee/index.htm

FOR MORE DETAILS

 

 

 

15 Miners at Nyarugusu have been rescued, they are all alive.

Displaying IMG-20170129-WA0048.jpg
15 Miners in one of the Nyarugusu area Mine in Geita Region, North west of Tanzania have been rescued after being under the mine since 26 January 2017 following a collapse of mound of soil that blocked the passage. Rescue efforts were tirelessly going since the incident were reported. All the rescued miners survived and were taken for further medical checkup and examinations.


Uyui: Kurasa za Mbele za Magazeti (Front Pages of Today’s Daily Papers in Tanzania)

 

 

 

Uyui

A website about Uyui, Tabora heritages and the Wanyamwezi

Shahermohd's Blog

Just another WordPress.com site

WordPress.com

WordPress.com is the best place for your personal blog or business site.