Mzee Hassan Rajab Waitume wa Chemchem


The late Sheikh Hassan Rajab, one of the most respected Tabora Senior Citizen in a picture with some family members at chechem Tabora
The late Sheikh Hassan Rajab, one of the most respected Tabora Senior Citizen in a picture with some family members at chechem Tabora

HASSAN RAJAB WAITUME

by Maganga Feruzi

 

Mchezaji wa zamani wa gossage na sunlight Hassan Rajab Waitume (83) amefariki dunia na kuzikwa nyumbani kwake chemchem,  mjini Tabora juzi.

 

Mmoja wa watoto wa marehemu Mashaka Hassan alilifahamisha  Uyui blog kwa njia ya simu kuwa marehemu alifariki baada ya kuugua kwa muda mrefu ambapo alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu na kupata matibabu wilayani  Kahama kabla ya kufikwa na kifo.

 

Katika uhai wake  hayati  Hasssan Rajab aliwahi kuchezea timu ya mkoa wa Tabora enzi hizo jimbo la magharibi katika kombe la sunlight (kombe la Taifa)  na Goisage kuanzia mwaka 1940 hadi 1966.

 

 Hassan akiwa anatokea  kampuni ya Reli ya Afrika mashariki, kituo cha Tabora karakana ya Rufita alikuwa akichezea namba tisa kwenye timu ya mkoa wa tabora  ambao wakati huo ikijulikana kama western province akiwa na akina Herry Hamisi ambaye naye amefariki, Juma mrisho na Iyunge mwanaSali.Iyunge anakumbukwa sana na wakazi wa tabora kwa mashuti yake.

 

Mashaka amesema kwamba pamoja na kuchezea timu ya taifa alikuwa anachezea timu ya Reli na akiwa na wenzake waliiletea vikombe vingi timu yao ya Reli Tabora.

 

Rajab ambaye siku zake za mwishoni alijikita katika dini akiwa imamu  Masjid Amman alikuwa ni sheikh wa wilaya ya tabora kuanzia mwaka 1989 hadi alipofariki.

 

Marehemu Rajab ameacha watoto 11 na wajukuu 16

Advertisements

One Response to “Mzee Hassan Rajab Waitume wa Chemchem”

  1. Shaib Says:

    INNALILAHI WAINNAILAIH RAJIUN MZEE WETU HUYU, NA NI KATIKA FAMILY NILIKUA SINA HABARI, MUNGU AMPE UJIRA NA TULIOBAKI TUTAENDELEA KUMUOMBEA NA KUWAOMBEA WAZEE WETU WALIOTANGULIA NA INSHAALAH MUNGU ATAZIPOKEA DUA ZETU,
    SHAIB.


Leave a Reply (Please be decent) Acha ujumbe wako hapa (kuwa mstaarabu)

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Uyui

A website about Uyui, Tabora heritages and the Wanyamwezi

Shahermohd's Blog

Just another WordPress.com site

WordPress.com

WordPress.com is the best place for your personal blog or business site.

%d bloggers like this: