Tabora tobacco farmers urged to have a cooperative bank


Spika wa Bunge, Samuel Sitta amesema kuna haja kwa wakulima wa tumbaku mkoani Tabora kuanzisha benki ya ushirika ili iweze kuwakomboa kiuchumi na kijamii.

Amesema kuanzishwa kwa benki hiyo kutakuwa ukombozi kwa wakulima hao na wataondokana na dhana ya utegemezi wa ukopeshaji wa pembejeo kila mwaka.

Kauli hiyo imetolewa na Spika Sitta wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Wakulima wa Tumbaku Kanda ya Magharibi (Wetcu) mjini hapa.

‘‘Wakulima mtakopeshwa pembejeo hadi lini? Kwani nini msiwe na chombo chenu kitakachoweza kuwakopesha pembejeo na wanunuzi wa tumbaku mkutane kwenye masoko tu,’’ alisema Sitta.

Alisema kwamba wakati sasa umefika wa kuwa na chombo kitakachomsaidia mkulima na kumkopesha ili kampuni zibaki na kazi moja tu ya kununua tumbaku.

Hata hivyo, Sitta akiongelea suala la mazingira alisema kwamba wadau wote wa tumbaku mkoani hapa kuhakikisha kuwa wanapanda miti kwa wingi bila ya kuchoka.

Alisema kwamba iwapo mtu hataki kupanda miti Bodi ya Tumbaku itumie sheria na kanuni zilizopo kumdhibiti na ikiwezekana afutiwe usajili ili asijihusishe tena na kilimo cha tumbaku.Aidha aliongeza kwa kusema kuwa muda mwafaka umefika kwa vyama vya ushirika vya msingi navyo kuwa na mashamba ya mfano ya miti.

 
Advertisements

Leave a Reply (Please be decent) Acha ujumbe wako hapa (kuwa mstaarabu)

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Uyui

A website about Uyui, Tabora heritages and the Wanyamwezi

Shahermohd's Blog

Just another WordPress.com site

WordPress.com

WordPress.com is the best place for your personal blog or business site.

%d bloggers like this: