Buriani Maina “Barnabas” Joseph


 

 

Buriani Maina “Barnabas” Joseph

 

Bonge, Sikujua kama ulikuwa na  kipaji cha uimbaji.

                                               

Siwezi kusema kwamba nilikufahamu sana Maina, lakini nilikutana na wewe mara ya kwanza miaka 30 iliyopita kule Tabora wakati huo tukiwa vivulana fulani hivi, tulikuwa kidato kimoja na tulisoma wote lakini sikubaini kama ulikuwa na kipaji cha uimbaji. Ulinipiga bao!

 

Unakumbuka mihogo ya mzee Amiri ilivyokuwa na pilipili unga, pamoja na sambusa za pale Kassu hoteli. Unakumbuka pia madisco au buggi la nmchana kule shule ya wasichana ya Tabora? Katika siku zote tulizokuwa shule sikuwahi kukuona unaimba au kuonyesha kipaji kuwa siku moja ungekuwa muimbaji.

 

Unakumbuka jinsi wakati huo mambo ya ushabiki wa ubaharia yalivyokuwa yameshika kasi sana kiasi kwamba darasani kwetu tulifunga jiwe tukimaanisha ile ile ilikuwa ni meli iliyotia nanga? Wengi walipenda wawe kama marehemu Mkai ambaye naye alikuwa mgosi lakini ndugu upande mwingine alikuwa mnyamwezi. Si unajua mgosi kuwa sisi ni baba zenu?

 

Wakati ule wa uanafunzi wetu ni fansis peke yake ndio alikuwa mwanamuzi pekee aliyekuwa anapiga gita katika bendi ya Tabora Jazz. Unakumbuka siku ya mahafali “graduation” pale shule ya sekondari ya Kazima, bendi ya Tabora Jazz ilikuja kupiga na Fransic akapanda jukwaani na sare zake za shule kupokea gitaa. Zilikuwa siku za kukumbuka bonge Maina. Wakati ule maisha yalikuwa mazuri mno.

 

Mijadala yetu enzi hizo ilikuwa ni masomo na mtu anapenda upande gani wa vita baridi vya duni. Je ni Urusi au Marekani. Wakati mwingine hilo lilituchukulia muda lakini pengine ulikuwa ni ujana mzuri ambao jioni tulikuwa tunaenda kituo cha wanafunzi “student centre” au uwanja wa chipukizi wa Padre Damiano kuangalia kabumbu la vijana.  

 

Sisi wengine tulikuwa watu wa  fujo fujo lakini wanafunzi wengi walikuwa wanapenda sana kijiwe chako, kwa sababu ya stori zako nzuri na zile za peter mwizarubi ambazo kwa kweli zilikuwa ni za kusisimua. Hakuna aliyejua kama ulikuwa ulikuwa unaitwa Maina Josheph. Wote tulikujua kwa jina la Maina Barnabas.

 

Unamkumbuka Amani? Yule aliyekuwa nyanda wa timu ya shule? Tulizoea kumuita “Dar es Salaam”. Tulimuita hivyo kwa sababu kila gari moshi lilipopiga kipenga cha kuondoka alikuwa anasema “aah Dar es salaam hiyo”. Hii ni kwa sababu shule yetu ilikuwa karibu mno na stesheni ya Tabora.

 

Pengine utakuwa umesahau kwa sababu siku nyingi zimepita lakini maeneo ya National, Kanyenye, Kalunde, Cheyo na maeneo ya Mihayo hasa pale jumba la Sinema la Diamond Talkies kwa yule bubu alikuwa anakaa mlangoni kama baunza, mitaa ambayo tulikuwa tukiipita mara kwa mara?

 

Tulipomaliza shule na  kutawanyika mungu bariki tukaja kukutana baadaye mitaa ya pugu road siku hizi barabara ya nyerere. Kila mmoja akacheka na kumshangaa mwenzeke. Haa bonge … haa bonge. Maina shuleni hukuwa bonge imekuwaje? Kila mmoja akacheka. Ukaniambia kuwa ulikuwa bendi ya National Panasonic. Nikakuuliza haya mambo vipi ndugu yangu. Ikawa wee acha tuu! Ulituficha kipaji chako mgosi Maina.

 

Baadaye ulipohamia Msondo tukawa tunaonana mara moja moja na ukanibadilisha niipende bendi hiyo. Unajua kuwa baadhi ya watu walikuwa haipendi msondo kule Tabora japokuwa waliiheshimu.

 

Watu walisononeka sana wakati Msondo ilipokuja Tabora miaka ya sabini mwishoni au themanini mwanzoni, pale Lumumba bar karibu na nyumba ya Ismail Rage kwa mama aden na baada ya kupiga muziki na Tabora Jazz.

 

Maina unakumbuka walipoondoka wakaondoka Issa Ramadhani (Baba Isaya) na Hamisi Kitambi ambao walikuwa vipenzi vya wana Tabora. Watu iliwauma kweli kweli. Hicho ndio kisa cha watu kupungua mapenzi yao kwa msondo. Ulipoingia wewe kutokea panasonic ulivuta baadhi ya watu nikiwemo mimi Maganga.

 

Kama ilivyokuwa kwa msondo watu pia walipunguza mapenzi yao kwa Mwenge Jazz, kisa walimchukua marehemu msafiri haroob. Baada ya kuizoea hiyo hali watu walianza kurudisha mapenzi yao kwa msondo na mwenge. Nadhani ni kitu ambacho hawakukizoea kuondokewa na wanamuziki waliowapenda.

 

Mara ya mwisho kuonana na wewe ilikuwa pale ukumbi wa Amana. Nilikuja kumuona mzee abdala kidule ambaye naye sasa ni marehemu. Tulicheka sana, kumbe ilikuwa ni kicheko cha mwisho.

 

Buriani Mgosi. Tabora yote inakulilia na kukumbuka. Kwa nini lakini ulinificha lakini. Tutaonana Bonge. Tangulia Maina, walikotangulia kaka zetu kina mwalimu Ngomeni, Ibrahim Marekano wa Kazima, Said Mwamba kizota wa Ng’ambo, Kasimu, Hanzuruni, msafiri haroob, Halfani Juma na Wema Abdalla waliokutangulia katika muziki  tabora ambao walipata kupigia  Tabora Jazz. Maina! siwezi kuendelea kuandika macho yamekuwa mazito, nimejawa na simanzi. magangaferuzi@gmail.com


 

 

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply (Please be decent) Acha ujumbe wako hapa (kuwa mstaarabu)

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Uyui

A website about Uyui, Tabora heritages and the Wanyamwezi

Shahermohd's Blog

Just another WordPress.com site

WordPress.com

WordPress.com is the best place for your personal blog or business site.

%d bloggers like this: