SITTA ASPIRES TO BOUNCE BACK TO SPEAKERS SEAT
SITTA AUTAKA USPIKA

ALIYEKUWA Spika wa Bunge la Tanzania lililomaliza muda wake, Samuel Sitta, ana hamu ya kuliongoza Bunge lijalo hivyo anatarajia kujaza fomu kesho kukiomba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimpitishe agombee uspika.
Sitta amesema, anafahamu kuwa Bunge lijalo litakuwa na changamoto zaidi kuliko lililopita, lakini ana uwezo na uzoefu wa uongozi hivyo atalimudu Bunge hilo la 10 la Tanzania.

Mwanasiasa huyo amesema, atafurahi kama atakuwa Spika wa Bunge lenye changamoto nyingi kama Bunge lijalo.
“Kwa kweli nadhani niseme wazi tu, wakati wangu ndiyo umefika” amesema Sitta wakati anahojiwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha ITV na Redio One Stereo saa kadhaa baada ya kutangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi wa ubunge jimbo la Urambo Mashariki kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alisema, anafahamu kwamba kutakuwa na wabunge wa kambi ya upinzani wenye uwezo mkubwa kisiasa, yupo tayari kuwaongoza, na pia atakaa vizuri na wabunge machachari ili kusiwe na vurugu bungeni.
“Hatuwezi kuwa na ukiritimba wa chama kimoja au viwili halafu tukasema hiyo ndiyo demokrasia…mimi natarajia tutaenda vizuri hasa wakinichagua kuwa Spika” alisema Sitta.

Source: Lukwangule.blogspot.com

Advertisements

Leave a Reply (Please be decent) Acha ujumbe wako hapa (kuwa mstaarabu)

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Uyui

A website about Uyui, Tabora heritages and the Wanyamwezi

Shahermohd's Blog

Just another WordPress.com site

WordPress.com

WordPress.com is the best place for your personal blog or business site.

%d bloggers like this: