Mwanamuziki mkongwe wa Tabora Jazz Rehani Juma afariki dunia


Mwanamuziki mkongwe Rehani Juma amefariki dunia usiku wa kuamkia jana
alfajiri akiwa anapatiwa matibabu hospitali ya mkoa ya Kitete, Tabora.

Taarifa kutoka jamaa wa karibu wa marehemu, Athumani Rehani zinasema kuwa
mwanamuziki huyo ambaye aliwika enzi za miaka ya 70 hadi 90 alifariki
dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Athumani alisema kwamba mwanamuziki huyo alikufa katika hospitali ya
Kitete Tabora ambako alikimbizwa kwa matibabu siku tatu zilizopita. Sababu
za kifo bado kutolewa na madaktari waliomhudumia.

Kwa mujibu wa taarifa hizo mwanamuziki huyo ambaye alitamba sana na kibao
cha Jullie kilichopigwa na bendi ya watunjatanjata (washirika) alizikwa
jana hiyo kwao Tabora katika maeneo ya Chemchem, karibu na shule ya
sekondari ya Milambo.

Rehani ambaye anatoka katika familia ya wanamuziki kabla ya umauti wake
alikuwa akiendelea na shughuli za muziki mjini Tabora akipiga rythimu na
solo katika bendi ya Tabora Sound wanasensema Malunde.

Rehani ambaye ni mdogo wa marehemu Khalfan Juma aliyekuwa anapiga gitaa la
besi katika bendi ya western kwa muda mrefu kabla hajajiunga na Tabora
jazz ,pia alishawahi kupigia Paselepa na akina Marehemu Msafiri Haroub
ambao wote wametoka Tabora.
Tabora Sound sensema malunde inaundwa na wanamuziki wengi waliofanyia
kazi katika bendi ya Tabora Jazz na kwa sasa inaongozwa na Madaraka Moris
maarufu kama baba kiwembe ambaye pia alikuwa Munisa Ndesa, na
watunjatanjata.
Tabora Sound inamilikiwa na mwanamuziki mkongwe aliyekuwa Tabora jazz
iliyotamba katika miaka 1970 Salum Ruzira ambaye alikuwa anapiga besi kama
anapiga ngoma, kama utafuatilia kwa karibu wimbo wa dada remmy.
mwisho

Advertisements

Leave a Reply (Please be decent) Acha ujumbe wako hapa (kuwa mstaarabu)

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Uyui

A website about Uyui, Tabora heritages and the Wanyamwezi

Shahermohd's Blog

Just another WordPress.com site

WordPress.com

WordPress.com is the best place for your personal blog or business site.

%d bloggers like this: