GULAM DEWJI REMTULLAH FOR TABORA MAYOR-SHIP


GULAM DEWJI REMTULLAH FOR TABORA MAYOR-SHIP

Kikao cha kamati ya Madiwani wa chama cha Mapinduzi kimemchagua diwani wa kata ya kanyenye mjini Tabora, Gulam Dewji Remtullah, kuwa meya manispaa ya Tabora kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Gulam,iwapo kama atathibitishwa kushika nafasi hiyo na baraza la madiwani katika kikao chake cha kwanza, atakuwa meya wa nne wa halmashauri ya manispaa ya Tabora toka ilipoanzishwa mwaka 1995, akitanguliwa na George Mpepo, Paul Misigaro na Peter Lembeli

Katika kikao hicho madiwani wa chama cha mapinduzi walimchagua mheshimiwa Gulam kwa kura 25 kati ya kura 32 za halali zilizopigwa katika uchaguzi huo ambao pia madiwani wengine wawili waliwania nafasi hiyo.

Madiwani waliojitokeza na kuwania nafasi hiyo sambamba na Gulam ni pamoja na katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi mkoani Tabora Idd Shaaban Kapama na Mrisho Shaaban Kaombwe.

Hata hivyo madiwani hao, waliambulia kura nne, alizopata Kaombwe na kura nyingine tatu alizopata katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi mkoa wa Tabora.

Diwani wa kata ya itetemia mjini Tabora, Haruna Kurwa ameteuliwa kuwania nafasi ya naibu meya wa manispaa ya Tabora na Selemani maganga kuwa katibu wa madiwani wa chama cha mapinduzi.

Kutokana na matokeo hayo Mheshimiwa Gulam, atathibitishwa kuwa meya wa manispaa ya Tabora, katika kikao cha kwanza cha baraza la Madiwani la Halmashauri ya manispaa ya Tabora,kinatorajia kufunguliwa na mkuu na mkuu wa mkoa wa Tabora, Abeid Mwinyimsa.

Kwa mujibu wa utaratibu mgombea wa kiti cha Umeya wa chama cha Mapinduzi atakuwa Gulam Dewji, ambaye atashindana na mgombea wa chama cha Demokrasia na Maendeleo ( Chadema), ambacho kimepata kiti kimoja cha Udiwani katika halmashauri ya manispaa ya Tabora.

Aidha kikao kama hicho kimependekeza jina la Mashaka Kalyuwa kuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya uyui mkoani Tabora, baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi uliofanyika leo.

Mashaka, aliwashinda mwenyekiti wa zamani wa halmashauri ya wilaya ya Uyui katika kipindi kilichopita Hamis Juma Bundalla na Haruna Salum Lwambo aliyejitokeza kuwania nafasi hiyo kwa mara ya kwanza. Huku Said Ntahondi akishinda nafasi ya makamo Mwenyekiti na Peter Mihayo akiwa katibu wa baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya hiyo.

Mwisho.

Advertisements

2 Responses to “GULAM DEWJI REMTULLAH FOR TABORA MAYOR-SHIP”

  1. gulf Says:

    gulam dewji naku wish good luck;GULF!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  2. Landan Stange Says:

    Thanks so much for the blog article.Thanks Again. Great.


Leave a Reply (Please be decent) Acha ujumbe wako hapa (kuwa mstaarabu)

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Uyui

A website about Uyui, Tabora heritages and the Wanyamwezi

Shahermohd's Blog

Just another WordPress.com site

WordPress.com

WordPress.com is the best place for your personal blog or business site.

%d bloggers like this: