Mzee Bomu wa Zinduka afariki dunia


Msanii mkongwe wa fani ya ngoma, maigizo na filamu nchini Abdallah Chembe Namulya (53) amefariki dunia.

Taarifa kutoka kwa jamaa wa karibu na marehemu Bw Hugo Martin Wagoma imesema kuwa marehemu Chembe amefariki dunia nyumbani kwakwe Tandale usiku wa kuamkia leo. Hata hivyo chanzo cha umauti wake hakikuweza kujulikana mara moja.

Marehemu Chembe maarufu kama Mzee Bomu alinyakulia umaarufu mkubwa katika sanaa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kupiga ngoma, kuimba, kufanya maigizo na kucheza filamu.

Kwa wasikilizaji wa kipindi cha Redio cha Zinduka kinachorushwa na TBC Taifa, Jina la Mzee Bomu si jina geni kwao. Katika filamu Mzee Bomu amejinyakulia umaarufu katika filamu ya HIFADHI yako na Joy zilizochezwa miaka ya 1990 chini ya Mtunzi mahiri wa filamu Hammie Rajab.

Katika uhai wake marehemu alifanya kazi katika kikundi cha Afro Dansi 1989 akiwa na Mzee Small wa Ngamba na baadaye alijiunga na Muungano ya Nobert Chenga kabla ya kufanya kazi na Simba theatre Group kwa muda na baadaye Kuwa miongoni wa waasisi wa Kikundi cha Ten Best cha jijini.

Kikundi cha Ten best kilitumika sana na Shirika la NSSF wakati wanabadili mfumo wao kutoka NPF huku Marehemu Mzee Bomu akichukua nafasi kubwa kama muelimishaji umma. Kikundi hicho kwa sasa kinafanya maonyesho mara moja moja na Bendi ya Muziki ya Msondo hapo Amana.

Kwa mujibu wa Hugo, Marehemu Mzee Bomu anatazamia kuzikwa kesho maeneo ya Vituka jijini.

Uyui inatoa pole nyingi kwa Familia ya marehemu Mzee Abdallah Chembe, ndugu Jamaa na marafiki kwa msiba huu mzito.

Advertisements

Leave a Reply (Please be decent) Acha ujumbe wako hapa (kuwa mstaarabu)

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Uyui

A website about Uyui, Tabora heritages and the Wanyamwezi

Shahermohd's Blog

Just another WordPress.com site

WordPress.com

WordPress.com is the best place for your personal blog or business site.

%d bloggers like this: