Mtangazaji wa zamani wa Radio Tanzania John Luwanda amefariki dunia Muhimbili jana mchana baada ya kuugua kwa siku kadhaa.Mtangazaji huyo wa zamani ambaye alistaafu kazi hiyo mwanzoni mwa miaka ya 1990 alikuwa amelazwa hospitali ya Muhimbili akisumbuliwa na kisukari huku akifanyiwa uchunguzi wakansa ya kibofu cha mkojo.Madaktari walimwambia kwamba baba yake alikufa kutokana na ugonjwa wa uti wa mgongo.Luwanda ambaye atakumbukwa zaidi na watu wa vikundi vya sanaa kwa uandalizi wa michezo ya kuigiza ya radio, mara baada ya kustaafu alikuwa anaishi katika kijiji cha Goba akilima bustani na kufuga.Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwake Gobakijijini na anatarajiwa kuzikwa Jumamosi wiki hii.Luwanda ameacha mke watoto 6 na wajukuu 20.
Uyui inatoa pole nyingi sana kwa Familia ya Mzee Luanda na kumuomba Mwenyezimungu awape nguvu na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu na cha majonzi.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina lake lihidimiwe Amina.
Uyui
Leave a Reply (Please be decent) Acha ujumbe wako hapa (kuwa mstaarabu)