NEWS ALERT: HAMMIE RAJAB AFARIKI DUNIA


HAMMIE RAJAB AFARIKI DUNIA


Mtunzi mahiri wa hadithi, mwandishi wa vitabu na muongozaji wa filamu Hammie Rajab (63) amefariki dunia.
Taarifa zilizoifikia Uyui muda mfupi leo hii, zimesema kuwa Marehemu Hammie amefariki jana usiku Dar es salaam na kwamba anatazamiwa kuzikwa nyumbani kwao Morogoro leo.

Marehemu Hammie alikuwa ni mtengenezaji filamu maarufu, mwandishi wa matangazo ya biashara na script za sinema, mwandishi wa vitabu na hadithi na Fundi wa magari (kazi ambayo wengi hawakupata kuifahamu).
Marehemu Hammie alipata elimu yake Morogoro na Nchini Kenya katika Mji wa Mombasa katika Taasisi ya MIOME ambako alifuzu na kutunikiwa cheti cha daraja la kwanza katika Motor Vehcle Technology. baada ya kufaulu vizuri mtihani wa united of Lancashire and Ceshire Insitutions(ULCI).

Hammmie aliajiriwa katika iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki upande wa Reli na Bandari kama fundi makanika, kazi aliyoifanya kwa miaka 7.

Hammie alijiunga katika Kampuni ya Filamu ya Tanzania (TFC) 1974 wakati huo wa kina Marehemu Elly Mboto kama Muongozaji wa filamu baada ya kupata mafunzo yaliyosimamiwa na Meneja uzalishaji wa kidenish Mr Tork Haxtausen.
Baadaye alienda nchini Kenya kwa ajili ya mafunzo zaidi. Baadhi ya kazi za mwazo alizozifanya ni pamoja na
BENKI YAKO (NBC)
MISITU NI UHAI( FORESTRY)
JIFUNZE KUSOMA
WATOTO WANA HAKI (UMATI)
USAWA (UMATI)
Marehemu HAMMIE ameandika vitabu vingi na script nyingi za filamu. Ameacha Mke na watoto.
Uyui inatoa pole nyingi kwa ndugu na familia.
Inna Lilahi wa Inna Ilayhi Rajeuun
.

Advertisements

Leave a Reply (Please be decent) Acha ujumbe wako hapa (kuwa mstaarabu)

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Uyui

A website about Uyui, Tabora heritages and the Wanyamwezi

Shahermohd's Blog

Just another WordPress.com site

WordPress.com

WordPress.com is the best place for your personal blog or business site.

%d bloggers like this: