FORMER YANGA BOSS MAHIMBO PASSED AWAY


THE LATE YANGA BOSS MZEE MAHIMBO

A TRIBUTE TO FORMER YOUNG’S AFRICAN BOSS: CHRIS MAHIMBO
The former Dar es Salaam Young’s Africa Secretary General in mid 1970s Christopher Mahimbo (82) passed away yesterday in Dar.

Godwin Mahimbo, a deceased son of the late Mahimbo told Lukwangule BlogSpot said his father’s death was caused by injuries he sustain after knocked by a car on 4th August, 2011.
The late Christopher Mahimbo was a Administrator, spiritual and sports leaders and for football fans he will be remembered by Young’s African for his courageous sprit to take leadership of the Club just after two years (in 1977) of the midst of crisis following the split of the club that resulted into Pan Africa football team in 1975.
During his lifetime Mahimbo worked in Tabora, Morogoro (at the then Institute of Development Management-IDM, now Mzumbe University) and in Dar es salaam where he was chief Boss of the old DMT (Dar es salaam Motor Transport) in 1973.
The late Mahimbo is survived by 10 children and at the time of his death he was a spiritual leader and a preacher.

KRISTOFA HERERI MAHIMBO WA YANGA AFARIKI DUNIA
ALIYEWAHI kuwa Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga, Kristofa Hereri Mahimbo (pichani) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kugongwa na gari.
Kwa mujibu wa taarifa ya mtoto wake Godwin Mahimbo, baba yake aligongwa na gari Agosti nne na kufariki saa saba usiku wa kuamkia jana.
Mipango ya maziko ya katibu mkuu huyo wa zamani inafanyika nyumbani kwake Makumbusho jijini Dar es Salaam.
Mahimbo atakumbukwa zaidi na wanachama wa Yanga kutokana na umahiri wake wakati wa kipindi kigumu cha Yanga cha mpito cha klabu hiyo kilichotokana na zogo lililoanzia mwaka 1974 na kusababisha Yanga kumeguka 1975.
Kumeguka huko ndiko kulikozaa Nyota ya Morogoro na baadaye Pan Africa.
blogu hii ambayo ilipata nafasi ya kuhoji watu kadha waliowahi kufanyanaye masuala ya michezo akiwamo Katibu Mkuu wa zamani wa Pan Africa, Mzee Mbwana Chombinga walisema wamesikitishwa sana na kifo chake kwa kuwa alikuwa mwanamichezo mahiri.
Mahimbo ambaye alisoma katika shule ya Mazengo sekondari wakati huo ikijulikana kama Alliance kabla ya kwenda Minaki,mpaka anakufa kwake alikuwa mweka hazina wa Tatedo. Aidha alisomea mambo ya serikali za mitaa huko Kabeta , Kenya na kufundisha Mzumbe kati ya mwaka 1967 na 1969.

Pia ameshashika nyadhifa mbalimbali serikalini na kutumikia katika mikoa Shinyanga, Tabora na kagera kabla ya kustaafu kwake na kujifunza uchungaji katika chuo cha Anglikana Korogwe kabla ya kuajiriwa na Jumuiya ya Kikristo mwaka 1976.

Aidha alishawahi kuwa Meneja mkuu wa DMT (Dar es salaam Motor Transport) shirika ambalo baadaye lilivunjwa na kuzaa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) na Kampuni ya Mabasi ya Taifa (Kamata) na yeye akabaki UDA. Aliteuliwa kuwa meneja mkuu DMT mwaka 1973.
Mahimbo ambaye ameacha mjane na watoto 10 alizaliwa mwaka 1929 mpaka anafariki alikuwa ni mhubiri mashuhuri wa dini.

mwisho

Advertisements
Posted in Soka. 1 Comment »

One Response to “FORMER YANGA BOSS MAHIMBO PASSED AWAY”

  1. Donasian Mbonea Says:

    Mzee Mahimbo alikuwa mchapa kazi na mpenda haki,na mabadiliko ya kisiasa nchini Tanzania,R.I.P Mzee Mahimbo.


Leave a Reply (Please be decent) Acha ujumbe wako hapa (kuwa mstaarabu)

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Uyui

A website about Uyui, Tabora heritages and the Wanyamwezi

Shahermohd's Blog

Just another WordPress.com site

WordPress.com

WordPress.com is the best place for your personal blog or business site.

%d bloggers like this: