MZEE KIPARA FUNDI SAID ATAKUMBUKWA


Msanii Mkongwe wa Maigizo na Filamu Mzee Fundi Said Maarufu kama Mzee Kipara (89) wa kwanza kutoka kushoto kwenye picha amezikwa jana katika makaburi ya Kigogo baada ya kuugua kwa muda mrefu. Mzee Fundi Said aliwahi kufanya kazi katika lililokuwa Shirika la Reli Tanzania (TRC) na blog hii ya Uyui ilianza kuvutiwa na kazi zake tangu miaka ya 1970 wakati aliigiza katika gazeti la filamu la picha lililojulikana kama Film Tanzania Magazine lililomilikiwa na Faraji Katalambula (Mzee Kipara alicheza kama Inspekta wingo katika filamu ya Simu ya Kifo iliyopigwa picha za Gazeti). Marehemu Mzee kipara pia alicheza michezo mingi ya kuigiza katika iliyokuwa Radio Tanzania (RTD) ampako alikutana na wakongwe wenzake wengine alkiwemo marehemu Mzee Hamisi Tajiri (Meneje Mikupuo), Ally Keto, Marehemu Mzee Ibrahim Raha (Mzee Jongo), Tunu Mrisho (Mama Hambiliki); Rajab Hatia; Ramadhani Mwanahewa; Majengo; Zena Dilip (Maua or Mama Hadia) na wengineo wengi ambako Marehemu Mzee John Luwanda na Salim Seif Nkamba walikuwa watayarishaji wa vipindi hivyo.

Marehemu Mzee Kipara hakuwa nyuma ya teknologia. wakati televisheni zinaanza Marehemu Mzee Kipara naye akaingia katika fani ya uigizaji wa tlevisihesni na michezo ya video. Aliigiza michezo mingi lakini Uyui inakumbuka sana filamu ya Simu ya Kifo iliyochezewa mjini Tabora ambako Mzee Kipara aliigiza kama Mzee Jacob.
Filamu ya Simu ya Kifo ilidhaminiwa na Dada Doroth Kipeja na kutengenezwa na Marehemu Hammie Rajab kutokana na simulizi ya kitabu cha simu ya kifo cha mzee Faraji Katalambula wa Igalula Tabora.
Marehemu Mzee Kipara pia alicheza filamu ya MLIMA KOLELO ya Irene Sanga ambayo pia ilitokana na kitabu cha Hammie Rajab cha Miujiza ya Mlima Kolelo na mpiga picha alikuwa Sylone Malalo.

Uyui inafahamu kuwa Mhe Mzee Sawel Sitta (MB) ambaye ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuwa ni miongoni mwa watu wachache wanaoweza kumuelezea vizuri Marehemu Mzee Kipara kwa sababu ya kutoka Sehemu moja Tabora na pili Mheshimiwa Sitta kuwa karibu zaidi na watu wa rika zote na hasa mapenzi yake kwa michezo na sanaa kwa ujumla. Kwa namna yoyote Mzee Kipara atakumbukwa sana na siku zinavyokwenda kazi zake zitapata umaarufu mkubwa kwa sababu alikuwa ni mmoja wa wasanii wa kwanza wa nchi hii aliyedumu katika fani hiyo akiwa kwenye kilele. Mwenyezi Mungu amuwie radhi, amsahamehe makosa yake na amuingize Peponi kwa rehema zake. Amina.

Advertisements
Posted in Film swahili. Tags: . 1 Comment »

One Response to “MZEE KIPARA FUNDI SAID ATAKUMBUKWA”

  1. Malcom Hecht Says:

    Admiring the commitment you put into your blog and detailed information you provide. It’s great to come across a blog every once in a while that isn’t the same old rehashed material. Fantastic read! I’ve saved your site and I’m including your RSS feeds to my Google account.


Leave a Reply (Please be decent) Acha ujumbe wako hapa (kuwa mstaarabu)

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Uyui

A website about Uyui, Tabora heritages and the Wanyamwezi

Shahermohd's Blog

Just another WordPress.com site

WordPress.com

WordPress.com is the best place for your personal blog or business site.

%d bloggers like this: