Uyui: Msanii wa Komedi Abadallah Salum SHOTI Afariki Dunia


Msanii wa maigizo ya vichekesho maarufu kama Komedi aitwaye SHOTI (30) amefariki dunia jijini Dar es salaam jana jioni majira ya saa 12 katika hospitali ya Mwananyamala.
Habari kutoka kwa msaani mwenzake wa karibu aliyekuwa akishirikiana naye Rashidi Omari au HASARA zimesema kuwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa vidonda vya tumbo kabla ya umauti kumkuta. HASARA amesema msiba uko maeneo ya Tandale karibu na kituo cha YEMEN na kwamba huenda akazikwa leo Jumamosi ama jijini Dar es salaam au kwao Mzenga. Enzi za uhai wake marehemu alikuwa maarufu katika sanaa ya maigizo ya Komedi na katikati ya miaka ya 2005 alikuwa akitoa burudani katika viwanja vya Leaders Club hasa siku za mwisho wa wiki wakati wa Bonanza ambako Bendi ya Twanga Pepeta ilikuwa ikiburudisha na yeye pamoja na mwenzake kupewa nafasi ya kuburudisha. Ameshiriki katika promosheni ya Taasisi kadhaa na kufanya vipindi katika baadhi ya Radio za FM hapa jijini Dar es salaam. Mwenyezi Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Abdalah Salumu.

Advertisements

Leave a Reply (Please be decent) Acha ujumbe wako hapa (kuwa mstaarabu)

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Uyui

A website about Uyui, Tabora heritages and the Wanyamwezi

Shahermohd's Blog

Just another WordPress.com site

WordPress.com

WordPress.com is the best place for your personal blog or business site.

%d bloggers like this: