Uyui:Best of Luck Candidates

Best of Luck candidatesToday is a significant day Tanzania’s 860,000 children who are sitting their Standard Seven national examination. The results will determine whether the candidates join Form One next year or the pitiful army of primary school dropouts.

It is a time of anxiety for parents too, for every mother and father wants their child to get a good education and, by extension, a promising life. Low income parents are probably the most nervous. They have the most to lose if their children do not make the grade for a place in public schools. Private school fees are famously well beyond the reach of the poor.source: the citizen newspaper

Uyui: Darasa la Saba kufanya mtihani leo (LY set for final exams today)

vijana wa darasa la saba wapatao 868,030 wanatarajia kuanza mitihani yao ya kumaliza elimu ya msingi leo.
kwa mujibu wa Radio ya Taifa TBC one, maandalizi yote muhimu yamekamilika ikiwemo usambazaji wa mitihani hiyo na karatasi za kujibia mitihani hiyo. Mtihani wa darasa la saba utafanyika kwa siku mbili na miongoni mwa masomo yatakayotahiniwa ni Kiswahili, Lugha ya Kiingereza na Maarifa ya Jamii.
Uyui inawatakia kila la heri wanafunzi wote wa darasa la saba wanaofanya mitihani yao leo hii. Kule Tabora tunawatakia mtihani mwema shule zote za Tabora hasa Chemchem, Rufita, Gongoni, Isevya, Uhuru (HR), Isike, Kazembe, Kazehill na Town school (sijui siku hizi inaitwaje) na nyinginezo nyingi. All the best Last year.L.Y

Uyui:Tanzania ya tatu kwa walevi wa ‘mataputapu’ Afrika (Gazeti la Mwananchi la leo)

Tanzania rank third in Africa for local brew consumptions. This story reminds Uyui about Kachome local brew grounds in Chemchem Tabora

Local Brew in tne making: Picture from Simbadeo.wordpress.com

Katika gazeti la leo la mwananchi kuna habari ambayo imekuwa ni ya kipekee na iliyovuta wengi ikiwemo vyombo mbalimbali vya habari hasa redio. Radio karibu zote zinazofanya mapitio ya magazeti wameisoma habari hii……… inasema hapa bonge asilimia 86 wanakunywa pombe za kienyeji kama wanzuki, rubisi, mbege, dadii, choya, moonshine, banana na gongo wakati ni asilimia 10 tu wanaokunywa bia na asilimia moja wanakunywa mvinyo wa viwandani, huku asilimia tatu wakinywa pombe nyingine kali zilizotengenezwa viwandani.

Kwa mchanganuo huo, wanaokunywa pombe za viwandani ni asilimia 14 tu ya wanywaji wote.

imekaririwa pia kuwa baadhi ya pombe huchanganywa na vilevi vyenye hatari kiafya kwa mfano anasema, methanol, ethanol au furfural inapozidi husababisha upofu na haitakiwi kunywewa na binadamu. Kwa kawaida pombe za kienyeji hutengenezwa kwa kusindika nafaka, na nafaka hizo zinapochachushwa hutengeneza vilevi(alcohol).

Imefahamika pia kuwa kiwango cha ‘alcohol’ hicho kimetofautiana kulingana na aina ya nafaka iliyotumika, kiwango cha joto kilichotumika kusindika na muda uliotumika kuchachusha pombe hiyo.

Habari hii inaikumbusha uyui eneo moja kule Tabora maneo ya chemchem mtaa wa Salmini ambako kulikuwa na Kilabu cha pombe kilichoitwa Kachoma na kule mitaa ya ng’ambo kama unaenda Tabora girls kulikuwa na vilabu lukuki vya pombe cha mateka wima na machwala. kwa sasa vilabu hivi havipo na kwa kweli pombe haifai kwani faida zake ni kidogo na hasara zake ni nyingi.

https://uyui.files.wordpress.com/2013/05/kufungia-stori-1.jpg?w=1042&h=47

Uyui: Tanzania News papers in nutshell (Magazeti ya Leo kwa Ufupi)

Yasemavyo Magazeti ya tarehe 5 septemba, 2013 kwa Ufupi(Today’s papers round-up).

JAMBO LEO

  • Maelfu wamzika Askofu Kulola: Askofu Mkuu wa Kanisa la Evengelical Assemblies of god Tanzania (EAGT) amezikwa jana na maziko yake kuhudhuriwa na maelfu. Marehemu alizaliwa Juni 2, mwaka 1928. Amefariki akiwa na umri wa miaka 85.
  • Jaji aonya waandishi: Jaji wa Mahakama kuu Tanzania, Fakih Jundu amewaasa waandishi wa Habari kuwa makini pindi wanapoandika Habari zinazohusu mahakama ili kuondokana na tatizo la kuingilia Uhuru wa mahakama.
  • Timbwili laanza YANGA. Wazee Yanga wamkataa Katibu Mkuu mpya
  • Cheka kutinga bungeni leo: Bingwa wa mkanda wa Shirikisho la ngumi la Dunia (WBF) uzani wa super middle, Francis Cheka leo atakuwa miongoni mwa wageni waalikwa katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

HABARI LEO

Wakili Magessa Afariki Dunia
Wakili maarufu na mkongwe, Israel Magesa amefariki dunia jijini Dar es Salaam jana.Msiba upo nyumbani kwa marehemu ukonga majumba sita ambako taratibu za mazishi zinaendelea.

Uyui: Grand Malt yamwaga vifaa Ligi Kuu Zenji

Grand Malt yamwaga vifaa Ligi Kuu Zenji

KINYWAJI kisicho na kilevi cha Grand Malt, walio wadhamini wa Ligi Kuu ya Zanzibar maarufu kama ‘Grand Malt Premier League’
jana walikabidhi rasmi vifaa kwa timu 12 zinazoshiriki ligi hiyo katika hafla iliyofanyika hoteli ya Bwawani, mjini hapa.
Mbali na kumwaga vifaa hivyo, Grand Malt pia wameamua kufanya kweli zaidi kwa kuongeza udhamini wao kwa waamuzi na uendeshaji wa ligi, ambapo msimu huu watatoa kiasi cha Sh milioni 200 kutoka Sh milioni 140 za msimu uliopita.
Hafla hiyo maalumu ya kukabidhi vifaa na kutangaza kiasi hicho kipya cha uendeshaji wa ligi, ilihudhuriwa na viongozi na wanamichezo mbalimbali wakiongozwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Saidi Ali Mbarouk.
source: Lukwangule.blogspot.com
Uyui

A website about Uyui, Tabora heritages and the Wanyamwezi

Shahermohd's Blog

Just another WordPress.com site

WordPress.com

WordPress.com is the best place for your personal blog or business site.