Uyui: Stesheni ya Igalula enzi hizo

Kufungia Stori 1

Ujiji ya Kigoma Utaipenda

 Tabora na Kigoma ni mikoa pacha yenye uhusiano na muingiliano wa mambo mengi tangu zamani hadi sasa. (picha ya Kapipi J habari)

https://uyui.files.wordpress.com/2013/05/kufungia-stori-1.jpg?w=1042&h=47

Uyui: Fundikira Road- Tabora

https://uyui.files.wordpress.com/2013/05/kufungia-stori-1.jpg?w=1042&h=47

uyui: SAUT Tabora Chuo Kikuu cha Mt Agustino-Tabora

https://uyui.files.wordpress.com/2013/05/kufungia-stori-1.jpg?w=1042&h=47

Uyui: Chuo cha Uhazili na Umaarufu wake Tabora

https://uyui.files.wordpress.com/2013/05/kufungia-stori-1.jpg?w=1042&h=47

Uyui: Lugha za Magari (Heshima Pesa Shikamoo Kelele tu!!!)

Uyui: Lugha za Magari

https://uyui.files.wordpress.com/2013/05/kufungia-stori-1.jpg?w=1042&h=47

Filamu: Baada ya miaka 200 Mzimu wa Waluguru wa Kolelo Watengenezewe filamu

Baada ya miaka 200 Mzimu wa Waluguru wa Kolelo Watengenezewe filamu

kolelo

Kolelo: Baada ya miaka 200, mzimu wa kiluguru wa karne ya 19  watengenezewa filamu ya kusisimua.

________________________________________________________________________________________________________

 Mzimu wa kolelo uliopo kwenye pango la mlima Kolelo umeichagua familia ya Kunambi kusika mikoba ili iweze kuwakomboa watu wa Lubasazi, Uluguru, Unguu, Duthumi, Vigolegole, kolelo, mvuha, Lukwangule na maeneo mengine kutokana na madhila,  kuwapa tiba ya maradhi  na kuwaongoza katika maombi pindi majanga mbalimbali yanapotokea. Komwe, mtoto wa Kunambi anasita kwenda mlimani kuchukua mkoba baada ya baba yake kufariki. Haikumsaidia. Alitumiwa mjumbe mlimbwende aitwaye Ndelawasi ili waende, aliposuasua mjumbe yule akabadilika ghafla na kuwa ajuza mwenye sura ya kutisha na Komwe hakuwa na namna nyingine pasi na kufunga safari ya kuelekea mlimani. Fuatana na mwandishi Maganga Feruz katika simulizi za filamu hii zinazosimuliwa na Shemeji wa Komwe, Mzee Juma wasiwasi katika Kolelo- filamu iliyotengenezwa na Irene Sanga, Sylone Malalo na Hammie Rajab.

­­­­­­­­­­­___________________________________________________________________________________________________________________

 Ukiiona kolelo utaipenda

Hata wale wavivu wa kuangalia, nina imani kuwa filamu hii itaisha kabla hawajachoka kuiangalia.  Ni filamu-simulizi fupi, pengine fupi zaidi kuliko zote ulizowahi kuzisikia, kuzijua  au hata kuziona. Ni muda wa kama dakika 38 tu hivi na ushee unakuwa umemaliza kuiangalia filamu yote!

Cha ajabu ni kwamba pamoja na ufupi huo, ukiiona, nina imani lazima utaipenda. Watengenezaji wake angalau wamejitahidi kuepuka mtego wa kuirefusha bila sababu, wakaifanya  isheheni matukio yote muhimu kwa ufupi lakini bila kuyaharakisha. Kwa lugha ya kiarabu filamu hii ingeweza kuitwa jumlat-lmufida, yaani Muhtasari unaojitosheleza.

Kolelo ni tofauti na filamu tulizozizoea

Filamu ya kolelo iko tofauti kidogo na filamu nyingi tulizozizoea. Humu kuna masimulizi ya karne ya 19 yanayoambatana na matukio mnasaba unayoyaona kwenye filamu yenyewe. Ni masilimuzi ya Mjomba anayemsimulia mpwaye kuhusu hisitoria ya wazazi wake, kuhusu chimbuko lao na hasa kuhusu mzimu wa Kolelo. Katika filamu hii  unapata simulizi inayoambatana na picha.

Simulizi za kolelo kwa Ujumla.

Kolelo, jina la Mzimu maarufu sana Morogoro. Asili yake ni jina la mwanamke Ajuza, Bibi aliyepewa karama na Mwenyezi Mungu ya kutibu na kutatua matatizo ya watu mbalimbali huko mlima Kolelo, kwenye pango ambapo mzimu wake ulifanya maajabu. Alipofariki, mzimu wake uliendelea kuwachagua watu wa kurithi mikoba. Kaburi la Bibi huyu lipo mpaka leo huko Lubasazi (Kolelo halisi). Ukilitaka waone walinzi wa Mlima Kolelo.

Zipo simulizi lukuki kuhusu miujiza ya Kolelo na mlima wenyewe, kubwa ni ile ya ufumbuzi wa matatizo ya Jamii. Ikitokea shida yeyote ya kijamii kama kukosekana kwa mvua, magonjwa, au hata shida binafsi mfano, kukosa mtoto kwa muda mrefu baada ya ndoa na kadhalika, watu wanakwenda katika mlima wa Kolelo na kufanya maombi (tambiko). Wakifika mlimani hapo  watalia, watoa machozi, watawaweka watoto wadogo na vikongwe mbele (hawa wanaaminika kuwa ni wasafi) na baadaye watachinja mnyama na kurudi. Kama ni shida ya mvua hawatafika nyumbani wakavu, watafika wamelowa chapachapa.

Ipo simulizi moja ya mapokeo isemayo kuwa, kulikuwa na  wanawake wawili ndugu walioenda kusenya kuni msituni, bila shaka karibu na mlima Kolelo. Mmoja akapotea, inasadikiwa alibebwa na joka hadi pangoni wakamtafutaaa… wakakata tamaa. Baada ya muda akatokea, akarudi akiwa na mkoba, mkoba wa Uganga! Ni mkoba huo aliorudi nao kutoka pango la Kolelo ndio alioutumia kuikomboa jamii dhidi ya madhila,  mkoba huu ukarithiwa kutoka kizazi hadi kizazi.

Ya Kolelo unaweza kusema ni ya zamani, lakini yapo ya sasa. Kama unaamini Mungu, basi jua kuwa kuna watu ambao Mungu amewapa karama. Juzi juzi tu hapa mlinzi mwingine wa milima ya Uluguru, Kingalu mwana Banzi wa 14 alisema haina haja ya Taifa kuingia gharama ya kutengeneza mvua na kwamba wao (kina Kingalu) bado wapo.

Kolelo ni mahala pasafi, wachafu hawafiki huko, ama sivyo wataumbuka. Sio uchafu wa mwili au mavazi, ni uchafu wa matendo na tabia. Ujumbe wa Kolelo ni kuwataka watu walirudie usafi wa matendo,  wazirudie mila na desturi. Kazi kweli kweli!

 Kolelo iliyotengenezewa filamu

Kama nilivyoeleza awali, zipo simulizi na matukio mengi yanayohusu Kolelo, Waluguru na mila zao zilizojaa urithi mwingi. Marehemu Mbaraka Mwinshehe Mwaruka aliwahi kuimba kuhusu Tambiko la Wahenga na wimbo mwingine wa Bondwa ugenda iii. Zipo simulizi za Kondoo wa Radi, na mambo ya milima ya unguu. Machache yamesemwa, mengi hayajasimuliwa wala kuandikwa. Urithi unapotea.

Filamu hii inatokana na kitabu cha Hammie Rajab, kiitwacho Miujiza ya Mlima Kolelo alichokiandika miaka ya 1980. Watengenezaji wa Kolelo wamechukua tukio moja tu,  la mtu na mkewe waliokaa muda wa muda takribani miaka mitano bila kubahatika kupata mtoto. Wenza hawa wakashauriwa. “kwanini hamuendi Kolelo? Wakaamua kufunga safari kwenda kolelo. “….. Unataka nikuambie kama walipata au hawakubahatika….? Mmh itafute Kolelo uone mwenyewe jinsi watoto wa mizimu wanavyokuwa au itafute filamu iitwayo Kibuyu.

Nilimuuliza mmoja wa Wakurugenzi wa filamu hii, Irene Sanga (mtunzi wa ule nyimbo ya salamu zangu kwako Mjomba) kwanini wameibana sana Kilelo kwa kuchagua tukio moja tu la mtu aliyetaka mtoto na wakaacha mengine kama ya mvua? Akanijibu kuwa wao wamechokoza tu! Watunzi wengine wanaweza kuibua Kolelo nyingine ikaogelea kitu kingine kwani matukio yapo mengi na kuyaeleza yoye kwenye filamu moja unaharibu ladha na kulipua kazi. Nilikubaliana na Irene Sanga, japo kwa shingo upande.

 Wahusika ndani ya filamu ya kolelo

Upo mseto wa majina makubwa na chipukuzi. Mzee Kunambi (Fundi Saidi/Mzee Kipara) yeye humu anayecheza kama mzee Kunambi. Huyu ni mkongwe katika fani. Yupo mama Thekla Mjata na Riama Ally (wanaocheza kama ndelawasi) wasanii wote hawa wamecheza pia filamu ya Simu ya Kifo iliyotengemezwa na Tripod Media ambayo nayo ni moto. Yupo Irene Sanga anayecheza kama mke wa Komwe (Issa Shamte), yumo Mrisho Mpoto na Issa Shamte (Komwe) anayecheza kama mtoto wa Mzee Kunambi anayetakiwa kurithi mikoba ya Kolelo. Ni wahusika wanaojua wanafanya nini. Hawapayuki kama wapo jukwaani.

Wamo pia wanakijiji wa Lubasazi, (lubasazi ndio Kolelo yenyewe)  ambao sina uhakika kama watabahatika kuiona filamu hii. Syllone Malalo ananitoa wasiwasi kuwa waliahidi kuirudisha Kolelo kwa wenyewe ili waione. Natamani iwe kesho!

 Upigaji wa picha,  na mandhari.

Picha za filamu hii zimepigwa na kuhariririwa na Syllone Malalo. Malalo ni mmoja wa watu anayeijua vilivyo kazi yake. Ni mbunifu. Katika Kolelo amejitahidi kuonyesha madhari halisi huku akibadili mikao ya kamera (camera angles)  kwa ustadi mkubwa. Ninathubutu kusema kuwa amefanikiwa kurudisha akili za watu kifikira kurudi vijijini walikotoka. Nyumba za udongo, taa za koroboi, hali ya kijani kibichi, uoto wa asili. Mavazi ya heshima. Lugha zisizo na mchanganyiko kwa kiswa-kingereza na mengineyo mengi.

Hadhari kubwa imechukuliwa kulinda uasili wa Kolelo ambayo, asili yake ni masimulizi yaliyorithishwa kutoka kizazi hadi kizazi kutokea karne ya 19 au hata nyuma yake. Upigaji picha wake pia unafuata mkondo huo huo. Upigaji picha wa aina hii hutumika kuelezea au kuonyesha matukio ya zamani za kale. Kwa ufupi Kolelo ni filamu-jarida au kama ni lazima kusema Kiingereza ndio ieleweke basi hii ni Documentary-film au kwa ufupi ina muundo wa Docu-film.

 Midundo na mirindimo inayosisimua.

Katika Kolelo kumepigwa sana mbeta, mbeta la kiluguru ambalo sasa hivi ukilitaka labda ufungulie RTD (tumbizo asilia), Radio Uhuru (karibu wataanza) TVT (ngoma zetu) au Radio Tumaini (chimbachimba muziki asilia na Che-Mundugwao) vinginevyo endelea na nyimbo za kimagharibi. Ipo siku nao watapiga nyimbo zetu!?

Wanaopenda ngoma asilia hasa zumari la mbeta, kwenye Koleo hapo watakuwa wamepata ile kitu roho inapenda. Mirindimo ya  ngoma hiyo pamoja na muziki uliotungwa na Irene na Msangi wenye mahadhi ya Reggae ya asili, roots ndivyo vinavyofanya mseto wa midundo murua ya zamani hadi siku hizi.

Nilimuuliza Irene kisa cha kuweka Reggae wakati filamu inaanza akaniambia kuwa wakati mwingine inabidi uchanganye na usasa kidogo uwavute watu wa rika zote hasa vijana wa leo.  Kwa hili sikukubaliana naye.

 Mila na tamaduni za kale

Katika mambo ambayo kina Irene  wanayojaribu kuyarudisha katika jamii ni ile mila ya kujizuia kufanya ngono hasa kwa mgeni ambaye hujamfahamu. Wanasisitiza ukarimu na msaada kwa mtu mwenye shida bila kumdai chochote kama malipo. Marehemu Hemed Maneti wa Vijana Jazz alishawahi kuimba kuhusu Chiapo, kuwa akimtendea  wema mtoto wa kike asijaribu kudai ujira wa mapenzi, a-jali asante.

Katika sehemu ya filamu hii tunamuona msichana, binti mzuri wa haja aitwaye Ndelawasi (Riyama Ally) kutoka Lukwangule, anapiga hodi kwa Komwe akiomba hifadhi. Anaomba msaada apelekwe Kolelo. Anakaa wiki nzima akila na kunywa bila kuombwa penzi.  Wote damu zinachemka lakini hakuna chuchuchu.

Kuna sehemu kolelo inatisha na kusisimua

Nani kasema wafu huwa wanarudi tena kuishi duniani? Nani ataamini kuwa kikongwe aliyofariki miaka kadhaa iliyopita tena akiwa na zaidi ya miaka 80 anaweza kujigeuza akaja kama binti mrembo wa miaka 18? Mbele ya macho yako? Si utachanganyikiwa? Uone binti anabadilika kuwa kikongwe halafu wakati huo huo anarudi kuwa msichana? Usikie ngurumo!!! Uone mlima unatikisika!! Haya ni baadhi tu ya matukio yaliyo ndani ya filamu hii. Utaogopa?

Yapo pia matukio ya  kuku kutoweka mikononi mwa aliyemshika na mtu kusikia sauti ambayo mwenza wake waliye jirani hasikii kitu kabisa.

Matukio ya kukumbuka nje ya filamu

Irene anasema safari ya kuelekea Kolelo kiasi inaogofya, kule hakuna mawasiliano ya mawimbi yeyote ya simu. Mungu bariki walisafiri salama kwenda na kurudi bila kuharibikiwa. Huku akionyesha kushukuru Mungu, anasema sijui ingekuwaje kama wangeharibikiwa kwa sababu hata magari kule yanapita kwa msimu.

Nilipomuuliza kuhusu mandhari ya Kolelo akasema alifurahia mambo mengi kikiwemo chakula cha kitoweo cha kuku wa kienyeji na sana alifurahia kuoga mtoni. Akaongeza kuwa kule wanaume wanaoga sehemu yao na wanawake wanaoga sehemu yao. Akakumbuka simulizi za moto mkubwa ambao uliishia kuuzunguka mlima miaka miwili iliyopita bila kuunguza hata jani la mlima. Akaongeza kuwa kuna wazungu walitaka kuingia mlimani bila kuomba ruhusa kwa walinzi wa mlima. Mpaka leo hawajulikani walikopotelea.

Kilio cha Irene Sanga

Kolelo ni zao la jitihada za Irene Sanga kutaka urithi wa Kolelo usipotee. Nilipata kumueleza Hammie Rajab kuwa Irene Sanga ni m-mila, akatasamu asinijibu kitu. Sikushangaa na wala yeye hakushangaa. Niliuliza swali ambalo jibu lake tayari nilikuwa nalo mkononi. Katika vita hii ya kuipigania urithi wetu, wapo makamanda ingawa sina uhakika na jeshi. Baadhi ya watanzania wapo, wapo watanzania mahiri kwelikweli  wanaojitahidi kudumisha mila na utamaduni kupitia sanaa katika mazungumzo yao, mavazi na fikra zao. Wapo wanakerwa na utamaduni wa kimagharibi.

 Kizazi cha luninga

Ipo hoja kwamba Sasa tupo katika Ulimwengu wa utandawazi huwezi kuishi kama kisiwa. Mimi sipingani na hoja hii. Swali ambalo najiuliza ni kuwa, huu utandawazi upo kwetu tu? Mbona Bara Hindi, Korea Kusini, Italia na kwingineko bado wanadumisha mila, utamaduni na urithi wao?

Najua ni vigumu, pengine ni ndoto ya mchana kurudia maisha ya uzamani. Marehemu Shaaban Robert alishawahi kuongelea ukale na usasa miaka kadhaa iliyopita. Kwa kuwa tumeziachia luninga ndio ziwalee watoto wetu pengine sisi hatuna muda wa kuwasilimulia wanetu hekaya na simulizi za mashujaa wetu kama mama Deborah Mwenda wa TVT na mama na mwana ya zamani RTD, basi angalau tuwanunulie  watoto na familia zetu kanda na filamu zinazoelezea asili na utaifa wetu.

 Kaditama

Nawahimiza watunzi na waja asili kama kina Merinyo wa Afrika sana, Benard Mapalala (kwa heri Iselamagazi), Ben Mtobwa na Mbogo (Ngome ya Mwanamalundi), Sisi Tambala, Mzee Jangala, Saidi wa Ngamba (mzee small), Farham Mohammed na Gumbo Kihorota (Itunyama) waendelee. Siwezi kuwataja wote orodha ni ndefu, lakini shime endeleeni. Potelea mbali, hata kama si leo iko siku vizazi vijavyo vitakuja kutanabahi na kuithamini asili, chimbuko na urithi wetu. Faraja ninayoipata ni kuwa angalau watakuwa na pa kuanzia kupitia filamu, wimbo, mavazi na simulizi zenu. Maasalamu.

https://uyui.files.wordpress.com/2013/05/kufungia-stori-1.jpg?w=1042&h=47

Uyui: Picha na Taswira za Mboka kwa nyakati tofauti

Uyui: Picha na Taswira za Mboka kwa Nyakati tofauti                                          

https://uyui.files.wordpress.com/2013/05/kufungia-stori-1.jpg

NSSF ILIANZA KUPENDEZESHA TABORA      Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Lilikuwa miongoni mwa Mashirika ya Mwanzo kabisa kuwekeza Tabora ujenzi mkubwa.

https://uyui.files.wordpress.com/2013/05/kufungia-stori-1.jpg?w=1042&h=47

CRDB TABORA           Benki inayosikiliza Mteja CRDB Nao hawako Nyuma, Ofisi yao inatazamana na Uliokuwa uwanja wa Chipukizi. picha kwa hisani

https://uyui.files.wordpress.com/2013/05/kufungia-stori-1.jpg?w=1042&h=47

 rafiki guest house      Enzi Hizooooo!!!!! Nyumba ya kulala Wageni iitwayo Rafiki. ilikuwa maeneo ya Stendi ya zamani ya Mabasi

https://uyui.files.wordpress.com/2013/05/kufungia-stori-1.jpg?w=1042&h=47

Kuelekea Isevya                                                                                                                       Kuelekea Isevya, hapa ni maeneo ya stesheni

https://uyui.files.wordpress.com/2013/05/kufungia-stori-1.jpg?w=1042&h=47

Uyui: Simulizi za Abuu Omari kuhusu Tabora: Unamkumbuka Afande Zakaria?

Uyui: Simulizi za Abuu Omari kuhusu Tabora: Unamkumbuka Afande Zakaria?                                          

Historia yake kwa ufupi:

Prof OmariMimi naitwa Abbu Omar, NI mwanamuziki wa kitanzania niishie Tokyo, Japan,Nina asili yangu pia ya Tabora, Babu yangu mzaa mama ni Mmanyema bibi yangu mzaa mama ni Mnyamwezi, Baba yetu alitoka kwao kusini akiwa kijana na kuloea Tabora pia kumuoa mama yetu nasi tukazaliwa Tabora. Nilisoma shule ya msingi Town primary school ( Town school) kuanzia 1970, dada zangu walikuwa wakisoma Hr primary school enzi hizo (Siku hizi Abuu shule hiyo inaitwa Mwenge shule ya mazoezi). Nikasoma sekondari Songea boys high school.

 Maisha ya muziki:

 Maisha ya muziki niliyaanza na Uda Jazz, Dares Salaam, na kuhamia Nairobi Kenya 1981, huko nilipigia bendi maarufu ya Simba Wanyika kwa miaka 10. Mwakaa 1992 nikahamia Tokyo,Japan hadi sasa nipo huku.

 Wazee Maarufu wa Tabora anaowakumbuka:

Mimi ni mjukuu wa marehemu Mzee Swedi Juma wa Gongoni, mjini Tabora, Mzee huyu nae tunaweza kusema alikuwa maarufu maana alikuwa referee mkubwa Tabora miakaya 68, 69,hadi 70. Kwa wapenzi wa soka wa enzi hizo watamkumbuka, pia alikuwa referee mkali sana.(Marefa wengine maarufu Abuu enzi hizo pamoja na  Mzee Hamisi Msonga, Marehemu Mzee Bundala na Chambera). Watu wengine maarufu Tabora ambao walikuwa katika ukoo wetu ni marehemu mjomba wetu Athumani Tembo (Baba Nyota) yeye alikuwa mpiga solo wa Tabora Jazz kabla hata ya Shem Karenga kuja Tabora kutoka Kigoma.

 Mjomba wangu mwingine mzee Juma Swedi ndio alikuwa mmiliki wa ofisi au palipokuwa na Club ya Sungura sports club,fundi street, (Abuu Sungura ilishaifungaga Yanga bao Moja kwa bila 1-0 mwaka 1973 habari zake zikangazwa Dunia nzima kupitia BBC, DW ya Ujerumani na Radio Burundi

 Wazee wengine mashuhuri waliokuwa karibu na familia yetu ni

  1. Mzee Iddi Shaha,
  2. Mzee Iddi Pazi,
  3. Mafundi cherehani maarufu mtaa wa ngoma
  4. Mzee Hassan Famba na
  5. Mzee Hamisi Mbuli,

 Askari Polisi Zakaria

Askari polisi maarufu mjini Tabora enzi hizo Zakaria. Huyu alijulikana ukali wake hasa ktk mechi za mpira wa miguu. (Abuu huyu Afande Alikuwa anatembea na pingu, Rungu na filimbi kama afande shap- Mkama)  Mzee Shabani Kilima ,Askofu Kisanji wa Moravian church.Familia ya akina Rage,Mama Rage na tanzania hotel.

Mtaa wa Usagara

MImi nilizaliwa hospitali ya KItete na nilikulia kona ya   mtaa wa usagara na ngoma  street nyumba yetu kubwa ya mawe, ilitazamana na Amani hoteli,kulikuwa na vinyozi,baadae ikawa Ngorongoro hoteli,baadae ikauziwa mchaga akafanya baa, hapo ndipo kwetu.hizi habari sana sana ni za enzi za utoto wangu miaka ya 69 kuja mwisho wa 70’s ILa baadae tulihama na mzee kwa ajili ya yeye kupata transfer.Wajomba na bibi bado wako Tabora.

Uyui: Kutokana na umahiri wa Abuu aliweza kuitwa Prof Jn na wapenzi wa muziki

https://uyui.files.wordpress.com/2013/05/kufungia-stori-1.jpg

Uyui: Mapozi ya Wadada wa Enzi zile

Pozi la Zamani makali yale yale 1

Pozi la zamani makali yaleyale

                                                          Uyui: Mapozi ya Wadada wa Enzi zile

Siku za nyuma, ukipiga picha lazima uweke pozi kama inavyoonekana kwa kina dada hawa. kitu kizuri ambacho kinaonekana kwenye picha hii ni staha. Wadada hawa wamevaa khanga ambazo ni vazi la staha na kwa kweli wamependeza. Wamependeza hawajapendeza?

vazi la khanga limekuwa likishika kasi yake hasa kwa kina dada wengi ambao wamegundua kuwa hilo ndio linawatoa zaidi katika mitoko ambayo huifanya ama kwenda kwenye shughuli au katika mambo yao ya kila siku.

https://uyui.files.wordpress.com/2013/05/kufungia-stori-1.jpg?w=1042&h=47https://uyui.files.wordpress.com/2012/11/alpha.jpg

Uyui

A website about Uyui, Tabora heritages and the Wanyamwezi

Shahermohd's Blog

Just another WordPress.com site

WordPress.com

WordPress.com is the best place for your personal blog or business site.