Uyui: Simulizi za Abuu Omari kuhusu Tabora: Unamkumbuka Afande Zakaria?


Uyui: Simulizi za Abuu Omari kuhusu Tabora: Unamkumbuka Afande Zakaria?                                          

Historia yake kwa ufupi:

Prof OmariMimi naitwa Abbu Omar, NI mwanamuziki wa kitanzania niishie Tokyo, Japan,Nina asili yangu pia ya Tabora, Babu yangu mzaa mama ni Mmanyema bibi yangu mzaa mama ni Mnyamwezi, Baba yetu alitoka kwao kusini akiwa kijana na kuloea Tabora pia kumuoa mama yetu nasi tukazaliwa Tabora. Nilisoma shule ya msingi Town primary school ( Town school) kuanzia 1970, dada zangu walikuwa wakisoma Hr primary school enzi hizo (Siku hizi Abuu shule hiyo inaitwa Mwenge shule ya mazoezi). Nikasoma sekondari Songea boys high school.

 Maisha ya muziki:

 Maisha ya muziki niliyaanza na Uda Jazz, Dares Salaam, na kuhamia Nairobi Kenya 1981, huko nilipigia bendi maarufu ya Simba Wanyika kwa miaka 10. Mwakaa 1992 nikahamia Tokyo,Japan hadi sasa nipo huku.

 Wazee Maarufu wa Tabora anaowakumbuka:

Mimi ni mjukuu wa marehemu Mzee Swedi Juma wa Gongoni, mjini Tabora, Mzee huyu nae tunaweza kusema alikuwa maarufu maana alikuwa referee mkubwa Tabora miakaya 68, 69,hadi 70. Kwa wapenzi wa soka wa enzi hizo watamkumbuka, pia alikuwa referee mkali sana.(Marefa wengine maarufu Abuu enzi hizo pamoja na  Mzee Hamisi Msonga, Marehemu Mzee Bundala na Chambera). Watu wengine maarufu Tabora ambao walikuwa katika ukoo wetu ni marehemu mjomba wetu Athumani Tembo (Baba Nyota) yeye alikuwa mpiga solo wa Tabora Jazz kabla hata ya Shem Karenga kuja Tabora kutoka Kigoma.

 Mjomba wangu mwingine mzee Juma Swedi ndio alikuwa mmiliki wa ofisi au palipokuwa na Club ya Sungura sports club,fundi street, (Abuu Sungura ilishaifungaga Yanga bao Moja kwa bila 1-0 mwaka 1973 habari zake zikangazwa Dunia nzima kupitia BBC, DW ya Ujerumani na Radio Burundi

 Wazee wengine mashuhuri waliokuwa karibu na familia yetu ni

 1. Mzee Iddi Shaha,
 2. Mzee Iddi Pazi,
 3. Mafundi cherehani maarufu mtaa wa ngoma
 4. Mzee Hassan Famba na
 5. Mzee Hamisi Mbuli,

 Askari Polisi Zakaria

Askari polisi maarufu mjini Tabora enzi hizo Zakaria. Huyu alijulikana ukali wake hasa ktk mechi za mpira wa miguu. (Abuu huyu Afande Alikuwa anatembea na pingu, Rungu na filimbi kama afande shap- Mkama)  Mzee Shabani Kilima ,Askofu Kisanji wa Moravian church.Familia ya akina Rage,Mama Rage na tanzania hotel.

Mtaa wa Usagara

MImi nilizaliwa hospitali ya KItete na nilikulia kona ya   mtaa wa usagara na ngoma  street nyumba yetu kubwa ya mawe, ilitazamana na Amani hoteli,kulikuwa na vinyozi,baadae ikawa Ngorongoro hoteli,baadae ikauziwa mchaga akafanya baa, hapo ndipo kwetu.hizi habari sana sana ni za enzi za utoto wangu miaka ya 69 kuja mwisho wa 70’s ILa baadae tulihama na mzee kwa ajili ya yeye kupata transfer.Wajomba na bibi bado wako Tabora.

Uyui: Kutokana na umahiri wa Abuu aliweza kuitwa Prof Jn na wapenzi wa muziki

https://uyui.files.wordpress.com/2013/05/kufungia-stori-1.jpg

Advertisements

4 Responses to “Uyui: Simulizi za Abuu Omari kuhusu Tabora: Unamkumbuka Afande Zakaria?”

 1. muharami j kayoka Says:

  daima ntamkumbuka baba yangu kipenz marehemu mzee juma hussein kayoka

  • uyui Says:

   Muharami
   Uyui knows how deeply sad we are following the departure of our beloved Mzee Juma Hussein Kayoka. Ni mzee aliyekuwa mstari wa mbele katika shughuli za maendeleo na mambo ya dini. Nakumbuka enzi za miaka ya 1980 ndiye mzee aliyekuwa na taxi (Kayoka cab,) Johari guest house bachu na duka soko kuu. Pia alikuwa mmoja wa wazee wa Msikiti wa Pale Salmin kwa Maalim Ismail Sandawatu. You are very luck to have Mzee Juma Hussein Kayoka as your father. Tumuombe duaa hasa sisi watoto kwa sababu dua ya mtoto kwa mzazi haina pazia. Stay blessed.

 2. NYALALI EMMANUEL MSHORO Says:

  Tabora is the home of tanganyika independence although it still poor in social,economically and politically. Msalimie mr mshoro.

  • uyui Says:

   Nyalali,
   Tabora will raise and its history will be lifted to unprecedented height. Its for Taborian to recite and promote the good image, immense contribution to the success of our Nation and let us go back and invest
   Uyui


Leave a Reply (Please be decent) Acha ujumbe wako hapa (kuwa mstaarabu)

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Uyui

A website about Uyui, Tabora heritages and the Wanyamwezi

Shahermohd's Blog

Just another WordPress.com site

WordPress.com

WordPress.com is the best place for your personal blog or business site.

%d bloggers like this: