Uyui: Ahmed Amasha (DC Suleiman Kumchaya ndiye alimpa Jina “Mathematician” Likadumu


"The Mathematician"

The Mathematician”

Ahmed Abdul Thabit Maarufu kama Amasha, ni mmoja wa wachezaji wachache mahiri ambao klabu ya Yanga na Taifa hili limeweza kuwapata katika historia ya Soka la nchi yetu. Beki Mahiri, mwenye akili na ujuzi ambaye ni mmoja wa Nyota kadhaa waliong’ara katika ulimwengu wa Soka la Tanzania wakitokea mkoa wa Tabora. Wengine wachache ni pamoja na Abdallah mwinyimkuu (Pele wa Gongoni) na Marehemu Said Mwamba Kizota (RIP), Hamis Kinye na wengineo wengi ambao wametikisha katika Anga la soka la nchi hii na hata nje ya mikapa.

Amasha, kutoka mtaa wa Salmini, chemchem Tabora ambaye alipata masomo yake ya Sekondari katika Shule ya Kazima ya Tabora alikuwa akiitwa mathematician kutokana na uchezaji wake mahiri lakini sio wengi wanaojua chimbuko la jina hilo. Jina hilo lilitokana na jinsi Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mheshimiwa Suleiman Omar Kumchaya wakati huo akiwa mtangazaji wa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) sasa hivi TBC TAIFA.

Ilikuwa ni katika mojawapo ya mechi za mpira wa mguu ambazo Mheshimiwa Kumchaya alikuwa akitangaza. lilitokea tukio moja ambao Ahmed Amasha alimpiga chenga mchezaji wa timu pinzani. Kwa namna aliyoipiga chenga ila Suleiman Kumchaya alitangaza redioni kuwa chenga ile kwa namna yoyote isingeweza kupigwa na mtu asiyejua hesabu. Alirudia kauli ile tena na tena na akasema kwa vyovyote iwavyo Ahmed Amasha ni lazima awe mwana mahesabu vinginevyo asingeweza kuipiga chenga ile. Tangu wakati ule jina la Mathematician likadumu na kustawi katika uchezaji wake mahiri katika soka.

Yapo mengi ya kujifunza kwa wachezaji wetu na yapo mengi ya kusimulia kutoka kwa vijana shupavu wa nchi hii wengi wakiwa kutoka Tabora ambao mchango wao katika Taifa letu utabaki kama kielelezo cha umahiri na kupigiwa mfano. Asante sana Ahmed Amasha Mathematician.

Advertisements

Leave a Reply (Please be decent) Acha ujumbe wako hapa (kuwa mstaarabu)

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Uyui

A website about Uyui, Tabora heritages and the Wanyamwezi

Shahermohd's Blog

Just another WordPress.com site

WordPress.com

WordPress.com is the best place for your personal blog or business site.

%d bloggers like this: