Uyui: All the Best Class IV (P.4) On your Examination Day (Kila la Kheri Darasa la Nne)

Uyui: All the Best Class IV (P.4) On your Examination Day (Kila la Kheri Darasa la Nne)

WANAFUNZI wa darasa la nne nchini kote  leo wanafanya mtihani wao wa kumaliza darasa la nne. Mtihani huu ni wa kwanza wa kifaita kwa wanafunzi hao ambao baada ya miaka 3 watalazimika kufanya tena mtihani mwingine ili kuhitimu elimu ya msingi watakapofika darasa la saba(last year au LY)

Kwa wale waliosoma enzi za Ukoloni darasa la nne la wakati ule lilikuwa na hadhi yake kwa sababu ili kuendelea na masomo katika elimu ya kati (Middle School), mwanafunzi alilazimika kufaulu mtihani wa darasa la nne.

Sisi UYUI tunawatakia kila la kheri vijana wetu ambao leo hii wanaifikia hatua yako muhimu katika maisha ya elimu.

Uyui: Tabora aiache kulalamika kukosekana soko la Embe: Ichukue Hatua kulitafuta

embe

Embe: Picha na Croppack Blog

Tabora aiache kulalamika kukosekana soko la Embe: Ichukue Hatua kulitafuta

Mwishoni mwa wiki iliyopita wakaazi wa Uyui mkoani Tabora walitoa kilio chao kuhusu kuoza kwa embe ambazo zinaonekana kukosa soko. Wakazi hao walitoa wito kwa wafanya biashara mbalimbali kujitokeza ili kununua zao hilo muhimu kwa chakula na biashara.

Wafanyabiashara wa zao la embe watafutwe na waombwe kufika Tabora

Sisi tunawaunga mkono, lakini tunawahimiza waende mbele hatua moja zaidi. Mfanya biashara na hasa mnunuzi wa mazo ya biashara haitwi kwa taarifa ya kwenye televisheni. Kama wafanyabiashara hao wanajulikana ni vyema waorodheshwe na wafuatwe na waombe kwa mazungumzo au hata kwa mawasiliano yoyote ikiwemo simu, barua pepe nk. Taarifa ya kwenye chombo japo inasikika sehemu kubwa lakini haiwezi kukuhakikishia kuwa yule uliyemlenga amepata ujumbe huo.

Jambo la pili ambalo ni kubwa zaidi ni kuilinda miembe

Tabora imebahatika kuwa na miembe mingi pengine kuliko mkoa wowote hapa nchini. Kwa sasa miembe ni mali. Bahati mbaya miembe hiyo inakatwa na kuchomwa mkaa. mwembe wa asili wenye umri wa zaidi ya miaka 10 unaukata mkaa ambao mbali na kuharibu mazingira unafinya fursa ya miembe hiyo kutumika kama zao la biashara. Kwa hali ya sasa ya ushindani wa biashara na ugumu wa zao la Tumbaku ambalo kwa kiasi kikubwa linaharibu mazingira. Tabora inaweza kabisa kugeukia zao la miembe. Ukitaka kujua soko la embe duniani angalia jinsi nchi ya India inavyonufaika. Sisi uyui tuna uhakika hata soko la ndani bado haijakidhiwa mahitaji yake.

Tanzia: Msiba Ikulu ya Unyanyembe ya Itetemia : Mzee Samwel Sitta (R.I.P)

The Late Hon Samwel Sitta (74)

The Late Hon Samwel Sitta (74)

Spika Msaafu na Mbunge wa Zamani wa Jimbo la Urambo Mashariki, Mzee Samwel John Sitta (74) amefariki dunia. Matangazo ya baadhi ya Televisheni yametakishwa ili kutoa habari hizo ambazo zimepokewa na majonzi makubwa. Taarifa mbalimbali zilizopo zinasema Marehemu Mzee Samwel Sitta amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Technical of Munich nchini Ujerumani alikokuwa akipata matibabu tangu mwezi uliopita.

Huu ni msiba mkubwa. Ni kazi ya Mwenyezi Mungu. Huu ni msiba mkubwa kitaifa lakini ni msiba mkubwa sana mkoani Tabora hasa ikulu ya itetemia kwa sababu Mzee Samwel Sitta ndio ujombani kwao. Sisi Uyui tunasema Inna Lilahi Waina Ilayhi Rajiuun. Huu ni msiba wetu sote. Tumeshindwa kuendelea, tuandike nini sasa!!!

Uyui: Form Four set for their final examination today

TODAY, its a historic day for the form four candidates all over the country as they start their final examination. To them and all others who went through this process one thing is evident ” a historic day”. Sitting in an examination room, is not something students would like to go for it or opting for. Unfortunately, there are very few and limited ways that have been developed and practiced, apart of from putting them in the examination room.

Our candid advise to student and parents is one. PREPARATIONS. Students should prepare for their examinations, read, understand and comprehend. In most cases, we do our things on a rush. We need to shift and change mindset and attitude of our children to start loving tests and get prepared for examination. The experience we went through this process is a lesson that will help our children to pass through this necessary stage in their life journey. We wish form four students all the best.

 

Uyui

A website about Uyui, Tabora heritages and the Wanyamwezi

Shahermohd's Blog

Just another WordPress.com site

WordPress.com

WordPress.com is the best place for your personal blog or business site.