Tanzia: Msiba Ikulu ya Unyanyembe ya Itetemia : Mzee Samwel Sitta (R.I.P)

The Late Hon Samwel Sitta (74)

The Late Hon Samwel Sitta (74)

Spika Msaafu na Mbunge wa Zamani wa Jimbo la Urambo Mashariki, Mzee Samwel John Sitta (74) amefariki dunia. Matangazo ya baadhi ya Televisheni yametakishwa ili kutoa habari hizo ambazo zimepokewa na majonzi makubwa. Taarifa mbalimbali zilizopo zinasema Marehemu Mzee Samwel Sitta amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Technical of Munich nchini Ujerumani alikokuwa akipata matibabu tangu mwezi uliopita.

Huu ni msiba mkubwa. Ni kazi ya Mwenyezi Mungu. Huu ni msiba mkubwa kitaifa lakini ni msiba mkubwa sana mkoani Tabora hasa ikulu ya itetemia kwa sababu Mzee Samwel Sitta ndio ujombani kwao. Sisi Uyui tunasema Inna Lilahi Waina Ilayhi Rajiuun. Huu ni msiba wetu sote. Tumeshindwa kuendelea, tuandike nini sasa!!!

Advertisements
Uyui

A website about Uyui, Tabora heritages and the Wanyamwezi

Shahermohd's Blog

Just another WordPress.com site

WordPress.com

WordPress.com is the best place for your personal blog or business site.