Uyui: Tabora aiache kulalamika kukosekana soko la Embe: Ichukue Hatua kulitafuta

embe

Embe: Picha na Croppack Blog

Tabora aiache kulalamika kukosekana soko la Embe: Ichukue Hatua kulitafuta

Mwishoni mwa wiki iliyopita wakaazi wa Uyui mkoani Tabora walitoa kilio chao kuhusu kuoza kwa embe ambazo zinaonekana kukosa soko. Wakazi hao walitoa wito kwa wafanya biashara mbalimbali kujitokeza ili kununua zao hilo muhimu kwa chakula na biashara.

Wafanyabiashara wa zao la embe watafutwe na waombwe kufika Tabora

Sisi tunawaunga mkono, lakini tunawahimiza waende mbele hatua moja zaidi. Mfanya biashara na hasa mnunuzi wa mazo ya biashara haitwi kwa taarifa ya kwenye televisheni. Kama wafanyabiashara hao wanajulikana ni vyema waorodheshwe na wafuatwe na waombe kwa mazungumzo au hata kwa mawasiliano yoyote ikiwemo simu, barua pepe nk. Taarifa ya kwenye chombo japo inasikika sehemu kubwa lakini haiwezi kukuhakikishia kuwa yule uliyemlenga amepata ujumbe huo.

Jambo la pili ambalo ni kubwa zaidi ni kuilinda miembe

Tabora imebahatika kuwa na miembe mingi pengine kuliko mkoa wowote hapa nchini. Kwa sasa miembe ni mali. Bahati mbaya miembe hiyo inakatwa na kuchomwa mkaa. mwembe wa asili wenye umri wa zaidi ya miaka 10 unaukata mkaa ambao mbali na kuharibu mazingira unafinya fursa ya miembe hiyo kutumika kama zao la biashara. Kwa hali ya sasa ya ushindani wa biashara na ugumu wa zao la Tumbaku ambalo kwa kiasi kikubwa linaharibu mazingira. Tabora inaweza kabisa kugeukia zao la miembe. Ukitaka kujua soko la embe duniani angalia jinsi nchi ya India inavyonufaika. Sisi uyui tuna uhakika hata soko la ndani bado haijakidhiwa mahitaji yake.

Advertisements
Uyui

A website about Uyui, Tabora heritages and the Wanyamwezi

Shahermohd's Blog

Just another WordPress.com site

WordPress.com

WordPress.com is the best place for your personal blog or business site.