Tanzia: Bi Hadija Kamba(94) Shujaa wa TANU Mwenye Historia ya Kusisimua kutoka Tabora Afariki Azikwa Dar.

bi-khadija-kamba_94AKIITWA  Hadija Bint Kamba, Miaka 94 (Sasa Marehemu) Bint mrefu mweusi mwenye umbo lililosadifu unyamwezi, asili yake ni Tabora ndipo alipotokea Baba yake na Kigoma ndipo wazazi wa Mama yake walipotokea.

Ni kama ilivyo kwa familia ya Sykes, Bint Kamba alitoka katika familia mashuhuri jijini Dar es salaam katika miaka ya 1950s. Aliingia katika harakati za ukombozi akiwa bint mdogo mwenye malengo tofauti kabisa na yakipekee sana. Pamoja na kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya ukoloni tena akiuza roho kwani alikuwa ni Bint pekee wa kiafrika aliyeweza kujichanganya na wazungu, hivyo aliweza kupata siri nyingi za wakoloni na kuwasaidia wapigania uhuru wasikamatwe na wakati mwingine wasidhurike. Alifanya kazi hii kwa siri kubwa sana, kiasi kwamba hakuwa akijulikana sana kwa watu hasa wanaharakati..alikuwa mtu mwenye uwezo wa kipekee wa kutunza siri.

Mwaka 1955 akiwa na Bibi Titi na Bint Maftah walishirikiana kuunda Baraza la Wanawake Tanganyika ikiwa ni kikundi ndani ya TANU kilichokuwa kikitoa ushawishi kwa akina mama kuiunga mkono TANU.

Mwaka 1961 wakati wa Uhuru, Bint Kamba alikuwa ni mmoja wa timu iliyoundwa kubuni nembo ya Taifa (maarufu kama nembo ya ikulu ama nembo ya adamu na hawa ambayo mpaka sasa imeendelea kuwa alama kuu ya Taifa {baadhi ya waandishi wanamtaja kuwa yule mwanamke anayeonekana kwenye nembo hiyo ndiye Bint Kamba)

Novemba 2 ya Mwaka 1962 Mwalimu Nyerere alipotangaza kuunda Umoja wa Wanawake wa Tanganyika  (UWT) Bint Kamba alikuwa ndio mpanga mikakati na mfumo wa uongozi wa UWT.

Pamoja na kushiriki katika mapambano ya kudai uhuru akiwa msiri mkubwa wa Mwalimu Nyerere, Bint Kamba hakuwahi kushika nafasi yeyote ya kisiasa kwa kugombea ama kuteuliwa. Baada tu ya nchi kupata uhuru Bint Kamba alieleza kuwa LENGO lake limetimia na kwamba haitaji CHEO chochote.

Mwaka 1985 katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Mwalimu Nyerere akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) Pamoja na Baraza la Wazee wa Dar es salaam juu ya kung’atuka alimtaja mtu mmoja ambaye ni wa kipekee aliyeyashangaza maisha yake ya uongozi. Alimtaja Hadija Bint Kamba kuwa ni mwanaMAMA na MPAMBANAJI wa kipekee aliyeshiriki mapambano ya uhuru bila tamaa ya cheo. Mwalimu Nyerere alisema kuwa amekaa ikulu kwa miaka 25 na kila alipotaka kumteua, Hadija Bint Kamba aliendelea kubaki na msimamo wake kuwa HAKUPIGANIA CHEO bali alipigania HAKI na USAWA…alitaka kuona Mwafrika anathaminiwa katika nchi yake na kwamba ametimiza LENGO hilo.

Tangu Mwaka huo wa 1985, Mwalimu alimtangaza Bint Kamba kuwa ni Shujaa asiyevaa Nishani, na tangu wakati huo alishirikia vikao vya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mikutano Mikuu yote akiwa ni mwalikwa mpaka pale umri ulipokuwa mkubwa na kumfanya ashindwe kuhudhuria vikao na mikutano hiyo.

BIBI HADIJA BINT KAMBA amefariki jana tarehe 30/11/2016 akiwa ni miongoni wa waasisi waliobahatika kuishi kwa muda mrefu katika nchi huru ya TANZANIA.

Bint Kamba amezikwa mchana wa Leo tarehe 1 Desemba 2016 katika makaburi ya Kisutu yaliyopo jijini Dar es salaam.

Anakufa bila CHEO lakini anazikwa kwa heshima ya KIONGOZI wa kitaifa, kwa msafara wa Magari ya askari na viongozi wa Chama na Serikali kutoka mtaani kwake mtaa wenye jina lake Bint Kamba street Ilala Bungoni mpaka Kisutu. Maraisi wastaafu, Katibu Mkuu wa Chama, Naibu Katibu mkuu na Viongozi  wengine wa Chama wakiongoza jeneza lenye mwili wake.

Anakufa bila UTAJIRI lakini anazikwa kwa HADHI ya Bilionea.

HIVI NDIVYO ULIVYO MWISHO WA WATU WEMA…!!!

CHANZO: Picha na Bashiri Nkoromo, Maelezo vyanzi mbalimbali

Advertisements

Uyui: Simulizi za Abuu Omari kuhusu Tabora: Unamkumbuka Afande Zakaria?

Uyui: Simulizi za Abuu Omari kuhusu Tabora: Unamkumbuka Afande Zakaria?                                          

Historia yake kwa ufupi:

Prof OmariMimi naitwa Abbu Omar, NI mwanamuziki wa kitanzania niishie Tokyo, Japan,Nina asili yangu pia ya Tabora, Babu yangu mzaa mama ni Mmanyema bibi yangu mzaa mama ni Mnyamwezi, Baba yetu alitoka kwao kusini akiwa kijana na kuloea Tabora pia kumuoa mama yetu nasi tukazaliwa Tabora. Nilisoma shule ya msingi Town primary school ( Town school) kuanzia 1970, dada zangu walikuwa wakisoma Hr primary school enzi hizo (Siku hizi Abuu shule hiyo inaitwa Mwenge shule ya mazoezi). Nikasoma sekondari Songea boys high school.

 Maisha ya muziki:

 Maisha ya muziki niliyaanza na Uda Jazz, Dares Salaam, na kuhamia Nairobi Kenya 1981, huko nilipigia bendi maarufu ya Simba Wanyika kwa miaka 10. Mwakaa 1992 nikahamia Tokyo,Japan hadi sasa nipo huku.

 Wazee Maarufu wa Tabora anaowakumbuka:

Mimi ni mjukuu wa marehemu Mzee Swedi Juma wa Gongoni, mjini Tabora, Mzee huyu nae tunaweza kusema alikuwa maarufu maana alikuwa referee mkubwa Tabora miakaya 68, 69,hadi 70. Kwa wapenzi wa soka wa enzi hizo watamkumbuka, pia alikuwa referee mkali sana.(Marefa wengine maarufu Abuu enzi hizo pamoja na  Mzee Hamisi Msonga, Marehemu Mzee Bundala na Chambera). Watu wengine maarufu Tabora ambao walikuwa katika ukoo wetu ni marehemu mjomba wetu Athumani Tembo (Baba Nyota) yeye alikuwa mpiga solo wa Tabora Jazz kabla hata ya Shem Karenga kuja Tabora kutoka Kigoma.

 Mjomba wangu mwingine mzee Juma Swedi ndio alikuwa mmiliki wa ofisi au palipokuwa na Club ya Sungura sports club,fundi street, (Abuu Sungura ilishaifungaga Yanga bao Moja kwa bila 1-0 mwaka 1973 habari zake zikangazwa Dunia nzima kupitia BBC, DW ya Ujerumani na Radio Burundi

 Wazee wengine mashuhuri waliokuwa karibu na familia yetu ni

 1. Mzee Iddi Shaha,
 2. Mzee Iddi Pazi,
 3. Mafundi cherehani maarufu mtaa wa ngoma
 4. Mzee Hassan Famba na
 5. Mzee Hamisi Mbuli,

 Askari Polisi Zakaria

Askari polisi maarufu mjini Tabora enzi hizo Zakaria. Huyu alijulikana ukali wake hasa ktk mechi za mpira wa miguu. (Abuu huyu Afande Alikuwa anatembea na pingu, Rungu na filimbi kama afande shap- Mkama)  Mzee Shabani Kilima ,Askofu Kisanji wa Moravian church.Familia ya akina Rage,Mama Rage na tanzania hotel.

Mtaa wa Usagara

MImi nilizaliwa hospitali ya KItete na nilikulia kona ya   mtaa wa usagara na ngoma  street nyumba yetu kubwa ya mawe, ilitazamana na Amani hoteli,kulikuwa na vinyozi,baadae ikawa Ngorongoro hoteli,baadae ikauziwa mchaga akafanya baa, hapo ndipo kwetu.hizi habari sana sana ni za enzi za utoto wangu miaka ya 69 kuja mwisho wa 70’s ILa baadae tulihama na mzee kwa ajili ya yeye kupata transfer.Wajomba na bibi bado wako Tabora.

Uyui: Kutokana na umahiri wa Abuu aliweza kuitwa Prof Jn na wapenzi wa muziki

https://uyui.files.wordpress.com/2013/05/kufungia-stori-1.jpg

Uyui: Msiba Mkubwa Tabora, Maalim Mtoro Juma amefariki Mazishi Jumamosi saa 10 Jioni

Tabora Lost one of his great Patron- Maalim Mtoro Juma

Uyui imepata habari za kusikitisha na huzuni kubwa leo asubuhi kwamba Mmoja wa Wazee muhimu na mashuhuri waliokuwa nguzo,. Maalim Mtoro amefariki dunia jana jioni. Taarifa kutoka tabora zinasema kuwa msiba uko nyumbani kwake maeneo ya Mtaa wa Zambezi nyuma ya Mwanza Road eneo la Gongoni. Taarifa zaidi ni kuwa mazishi yatafanyika Jumamosi saa 10 Jioni. Tumuombee sana dua mzee wetu huyu kazi aliyoifanya ni kubwa na tujiombee wenyewe.Inna Lilahi waina Ilaihi Rajiuun.

Tabora lost one his great  Patron Sheikh Mtoro Juma, popularly known as Maalim Mtoro. The late Maalim Mtoro was great scholarly and his used most of his lifetime to groom and upbringing the youth toward the right path of respects, ethical behavior and fearing Allah. He had a Madras which started  in 1960s. Sheik Mtoro passed away peacefully at Gongoni, Zambezi Street in Tabora Municipal. Let us raise and pray before Allah for his pardon and blessing so that Our Patron be awarded firdous for the dedicated lifework his deed for Tabora and Taborians.

https://uyui.files.wordpress.com/2013/05/kufungia-stori-1.jpg?w=1042&h=47https://uyui.files.wordpress.com/2012/11/alpha.jpg

Uyui: Former Tabora MP Siraju Kaboyonga Died at 64

Msiba Mzito waigubika tena Tabora. Yapoteza Mmoja wa Mashuja wake Muhimu Mzee Siraju Kaboyonga..

Mbunge wa Zamani wa Tabora Siraju Kaboyonga afariki Dunia

Mbunge wa Zamani wa Tabora Siraju Kaboyonga afariki Dunia

Mbunge wa Zamani wa Tabora (2005-2010) Mzee Siraju Juma Kaboyonga amefariki Dunia. Mheshimiwa Siraju alikuwa Mwanazuoni, Mwekezaji na mdau wa maendeleo ya Tabora, na pia mwanafunzi wa Kazima Sekondari(miaka ya 1960 mwishoni). Anatazamiwa kuzikwa leo katika makaburi ya kisutu Jijini Dar es salaam.Machozi na vilio vimetanda Mji wote wa Tabora. Inna Lilahi Waina Ilaihi Rajiuun.

Uyui: Homage to Fahim Ahmed:a brother, a Comrade and a friend of Tabora network

Sorry for the Picture but we have to pay A Tribute to Fahim Ahmed (Poley) Kanyenyela. The Great son of Tabora and our brother at Uyui.

The late Fahim Ahmed (poley)one of the great son of Tabora


Buriani Kaka Mkubwa Fahimu. Tabora itakukumbuka daima.

Taborians bidding a farewell to their loved brother

The great taborian of all times fahim ahmed (poley) son of kanyenyera, the owner and operator of Orion Tabora hotel passed away last week at the kitete hospital, tabora. Last Friday at 2.00 pm the funeral ceremony was made at the Orion Tabora Hotel Ground, followed by messages from well wishers, a funeral buffet lunch and finally entourage of his body to the Isevya grave yard. He will definitelybe missed by all of us, may the lord rest his soul in peace, amen. Thanks to Alnash Kasamal Murji for all the updates and thanks the tabora family Milton Mugambo, Fo’ said, Tabrez, Shaher Dinesh and all others.There is only one Tabora, a multi-cultural multi-racial society of the wanyamwezi with a strong social capital of all times..

Uyui: ten (10) things you will never found them anywhere except in Tabora, Mboka or Kazeh town

Ten (10) Uniqueness about Tabora, Mboka or Kazeh town.

Ten things you never knew about Tabora

 1. A town of Railways net work: Tabora is a hub of Railways providing gateways to Kigoma, Mwanza and Mpanda(Katavi) Regions;

 2. Tabora had its own currency– the Tabora rupees since the Germany era;

 3. The rational decision to enter into a referendum that gave Victory and later to Independence was made in Tabora in 1958;

 4. The two Tanzania Presidents the JKs i.e. Mwalimu Julius Nyerere (1st President) and the 4th Phase President Hon Dr Jakaya Kikwete  all worked in Tabora in 1950s and 1980s respectively;

 5. That Prominent Leaders in Sports, Politics and Sports came from Tabora. Some of them Include the late Chief Abdallah Fundikira, Kasanga Tumbo, Kasella Bantu, Said Maswanya, Samwel Sitta, Ibrahim Lipumba (The current CUF chair), Ismail Aden Rage (Former MP-Tabora) for a full list see Tabora celebrities

 6. Tabora was a center of Education (quality one) both conventional and theology. Itaga and Kipalapala are the Old and respectable RC seminary centers where as Teaching Centers by the Late Sheikh Rashid attracted many Islāmic Scholars e.g. the Chief Mufti Shaban Simba of Muslim Council of Tanzania who used to come and learn. Schools such Tabora Boys, Girls, Mirambo (St Marry) groomed most of the leaders in this Country.

 7. Tabora is a multi racial society dates over 100 years where the Arabs, Asians and   Europeans are all the Wanyamwezi and not ashamed of being Taborians.

 8. Prominent explorers and big names in the history e.g. Livingstone, Mohammed Said Almarjeb (Tipu- Tipu) had their stop over at Tabora;

 9. A Very Unique appreciation: No one who happened to live in Tabora and give it a negative publicity.    they all appreciated to be in Tabora during their lifetime;

 10. The Taborians (Wanyamwezi) are friends of all and they can easily get help in any Region in Tanzania because of historical ties established with other ethnic groups such as Wazaramo (watoto wetu hawa), waluguru, wandegereko (ndengestan), wamakonde, wagogo (walikuwa wanatufichia mizigo yetu tukipita pale Dodoma kwa mguu kuelekea Dar), Wahehe (walitaka kutupiga enzi za Mtemi Mirambo tukawapa dada zetu sasa hivi wanatuamkia kwa kuwa ni Shemeji na wajomba zao). Wangoni etc. From this relationship Tanzania has become a tribeless country and become a homogeneous   society that respects everyone regardless of tribe, religion and social economic status. God bless Tabora and Tanzania. 

        Above all Tabora is a honey town, don’t go to tabora and return without it. you                   wont be understood.

Uyui: Homage to Maalim Ahmada bin Salim

Msikiti wa Ijumaa Tabora

Buriani Maalim Ahmada Salim

Buriani Maalim Ahmada bin Salim.

Taarifa za msiba wa Maalim Ahmada nimezipata jana kuwa Tabora imeondokewa na mmoja wa Viongozi mashuhuri ambaye alikuwa Mwalimu wa Dini. Moja kati ya matunda ya kazi za mkono wake ni kuwa wanafunzi wake wameweza kuwa viongozi na wasomi wa kuaminiwa ndani na nje ya mkoa wa Tabora. Sheikh wa sasa wa Mkoa wa Tabora Sheikh Shaban Salum ni mmoja wa wanafunzi wake. Madrasa ya Marehemu Sheikh Ahmada Salim ni moja kati ya Madrasa kongwe mjini tabora tokea miaka ya 1960 na ilikuwa maeneo ya Ali Hassan Mwinyi Tabora. Inna Lilahi waina Ilaihi Rajiuune

TABORA LOST ONE OF THE GREATEST RELIGIOUS CLERICS MAALIM AHMADA SALIMU

One of the greatest son of Tabora and a relious clerics, Maalim Ahmada Salim passed away this week.Maalim Ahmada had a teaching school dated since 1960s and managed to groom his students to the highest level of knowledge and one of them is the current Regional Cleric of Tabora, Sheikh Shaaban Salum.

Maalim Ahmada had a Madrasa at Ali Hassan Mwinyi Area in Tabora Municipal. Rest in Peace the beloved and respect Ulamaa of Tabora.


magangaferuzi@gmail.com


Uyui

A website about Uyui, Tabora heritages and the Wanyamwezi

Shahermohd's Blog

Just another WordPress.com site

WordPress.com

WordPress.com is the best place for your personal blog or business site.