Hakuna aliyewahi kufikiria kuwa kuna siku Barabara ya Chaya hadi Nyahua itakuwa ya Lami

Unbelievable!!! Nyahua now to be tarmacked

Serikali ya Kuwait imeahidi kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Kimarekani Milioni 34 kwa ajili ya ujenzi wa barabara yenye urefu wa Kilometa 85 kwa kiwango cha lami kutoka eneo la Chaya hadi Nyahua mkoani Tabora.

Mwakilishi wa Balozi wa Kuwait hapa nchini, Bw. Mohammad Rashid Alamiri, aliyeongoza ujumbe kutoka Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait, amebainisha hayo jana wakati yeye na ujumbe wake alipomtembelea na kufanya mazungumzo Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya Tanzania na Kuwait.

Dkt. Mpango ameushukuru Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait (Kuwait Fund) kwa kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu utakaochochea maendeleo kwa Watanzania hususani wanaoishi maeneo hayo kutokana na umuhimu wa barabara katika kukuza uchumi wa Taifa.

Amesema kuwa kipande hicho cha barabara kutoka Chaya hadi Nyahua, ambacho kiko Barabara Kuu itokayo Dar es salaam kwenda katika mikoa ya Tabora na Kigoma, licha ya umuhimu wake katika kukuza biashara na usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo ikiwemo inayokwenda nchi jirani, ilikuwa haijapata fedha kwa ajili ya ujenzi wake.

“Nawahakikishia kuwa baada ya muda si mrefu wananchi wa mikoa ya Tabora na Kigoma watarajie kuona mkandarasi akiingia kazini ili kujenga barabara hii muhimu sana kwao na kwa uchumi wa Taifa kwa ujumla” Alisisitiza Dkt. Mpango.

Ameeleza kuwa ujenzi wa kipande cha barabara hiyo kutoka Chaya hadi Nyahua  unatarajia kugharimu shilingi Bilioni 61 lakini Kuwait haitatoa fedha zote hivyo ameuomba Mfuko huo uangalie uwezekano wa kutoa kiasi hicho chote cha fedha  ili uweze kukamilika mapema.

Uyui

A website about Uyui, Tabora heritages and the Wanyamwezi

Shahermohd's Blog

Just another WordPress.com site

WordPress.com

WordPress.com is the best place for your personal blog or business site.