Uyui: Tabora aiache kulalamika kukosekana soko la Embe: Ichukue Hatua kulitafuta

embe

Embe: Picha na Croppack Blog

Tabora aiache kulalamika kukosekana soko la Embe: Ichukue Hatua kulitafuta

Mwishoni mwa wiki iliyopita wakaazi wa Uyui mkoani Tabora walitoa kilio chao kuhusu kuoza kwa embe ambazo zinaonekana kukosa soko. Wakazi hao walitoa wito kwa wafanya biashara mbalimbali kujitokeza ili kununua zao hilo muhimu kwa chakula na biashara.

Wafanyabiashara wa zao la embe watafutwe na waombwe kufika Tabora

Sisi tunawaunga mkono, lakini tunawahimiza waende mbele hatua moja zaidi. Mfanya biashara na hasa mnunuzi wa mazo ya biashara haitwi kwa taarifa ya kwenye televisheni. Kama wafanyabiashara hao wanajulikana ni vyema waorodheshwe na wafuatwe na waombe kwa mazungumzo au hata kwa mawasiliano yoyote ikiwemo simu, barua pepe nk. Taarifa ya kwenye chombo japo inasikika sehemu kubwa lakini haiwezi kukuhakikishia kuwa yule uliyemlenga amepata ujumbe huo.

Jambo la pili ambalo ni kubwa zaidi ni kuilinda miembe

Tabora imebahatika kuwa na miembe mingi pengine kuliko mkoa wowote hapa nchini. Kwa sasa miembe ni mali. Bahati mbaya miembe hiyo inakatwa na kuchomwa mkaa. mwembe wa asili wenye umri wa zaidi ya miaka 10 unaukata mkaa ambao mbali na kuharibu mazingira unafinya fursa ya miembe hiyo kutumika kama zao la biashara. Kwa hali ya sasa ya ushindani wa biashara na ugumu wa zao la Tumbaku ambalo kwa kiasi kikubwa linaharibu mazingira. Tabora inaweza kabisa kugeukia zao la miembe. Ukitaka kujua soko la embe duniani angalia jinsi nchi ya India inavyonufaika. Sisi uyui tuna uhakika hata soko la ndani bado haijakidhiwa mahitaji yake.

Advertisements

Warembo wa Urambo Girls wa Mwaka 1966!!! (Picha ina umri wa miaka 50)

                           Young girls of Urambo Middle School in a picture 1966
This is the Picture of Young ladies of those old good days. It was taken in 1966 at Urambo Middle School and in the Pictures were the Prefects of the school. Am told most of them went to Tabora Girls and thereafter to colleges and by this time definitely they are senior Ladies.

Waliopo pichani ni waliokuwa wanafunzi wa shule ya Kati ya Wasichana ya Urambo. Picha hii ilipigwa mwaka 1966. Hawa walikuwa viranja wa Shule. wengi kati ya hawa waliendelea na masomo katika shule ya Sekondari ya Tabora na baadaye kwenye vyuo mbalimbali. Kwa sasa ni Dada Wakubwa.

Welcome “karibu” to Tabora (Mboka or Kazeh) and to Uyui- by Maganga Feruzi

The map of Tabora Tanzania, Mboka or Kazeh (magangaferuzi@gmail.com)

Thanks for visiting this site and you will never regret.Welcome to this wonderful and informative site of Uyui. Uyui is at the heart of Tabora Region (Young Generations called it- MBOKA and Elderly they used to KAZEH) in the western part of the United Republic of Tanzania. Not many people are aware of its beauty and the compassionate of its people. The Wanyamwezi, a popular tribe whose people are lovely and full of aptical culture that is demonstrated by their simple life. Wanyamwezi are the local residents of Tabora.Karibu (welcome) to Uyui so that you can learn the untold story and the wonderful lifestyle of Wanyamezi Tribe (Wanyanyembe, Wakonongo, Wasumbwa etc).

Write to us magangaferuzi@gmail.com  tuandikie magangaferuzi@gmail.com

Kufungia Stori 1

Uyui: Do you remember Kiwere saw mills? if not just read this from Roomina

Wow I stumbled across this site while searching for Kiwere Sawmills. My grandfather started the business and my dad and his brothers took over when he passed away. My family was very well known in Tabora in those days. Unfortunately, we left Tabora in Nov 1975.

How we all still mis home. It’s been 40 years but Tabora is still our home and in our hearts.

My brother and I both went to Uyui, he was in form 2 and I was in form 1 when we left. Some of my classmates were Tabrez, Safeer, Munisha , Saida and Priti. I’ve met Tabrez and have Munisha on my FB. Would love to know where the rest are.

I remember Amiri’s mogo (may his soul rest in eternal peace ) and I remember the stadium. My brother used to go there to watch the games. His favorite team was Simba.

Really miss those days

 

 

Uyui: Despite the distance some of Tanga Streets resemble Tabora

Tanga

For those who have visited the two Regions, there are some similarities in some of areas. We are not and definitely will not be history teachers, but we have learned some few. Both are historical towns down the lane since and even beyond Germany’s epoch, more precisely on the arrivals of Arabs.  Residents of Tabora and Tanga were used to traveling using Railways, but now its Tabora that still dominated by such kind of transport. Uyui found one street in Tanga to resemble some of the streets in Tabora. We are still finding out the connection between the two towns that distant apart.

Kwa wale waliotembelea mikoa hii miwili wataona kuna mfanano wa baadhi ya mambo. Sisi sio na kwa vyovyote hatutakuwa waalimu wa historia, lakini tumejifunza vitu vichache katika hili. Miji yote hii ni ya kihistoria na unaweza kuiangalia kuanzia enzi za Wajerumani na hata wakati wa ujio wa Waarabu. Wakazi wa Tabora na Tanga walizoea kusafiri kwa gari moshi (treni) lakini kwa sasa ni usafiri huo umebakia kuwa ni njia kuu kwa Tabora. Uyui imeona mtaa mmoja hapo kwenye picha ambao unafanana na baadhi ya mitaa ya Tabora na bado tunaendelea kuangalia uhusiano uliopo kati ya miji hii miwili ambayo imetanganishwa na umbali mrefu zaidi.

Kufungia Stori 1

Uyui: Picha na Taswira za Mboka kwa nyakati tofauti

Uyui: Picha na Taswira za Mboka kwa Nyakati tofauti                                          

https://uyui.files.wordpress.com/2013/05/kufungia-stori-1.jpg

NSSF ILIANZA KUPENDEZESHA TABORA      Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Lilikuwa miongoni mwa Mashirika ya Mwanzo kabisa kuwekeza Tabora ujenzi mkubwa.

https://uyui.files.wordpress.com/2013/05/kufungia-stori-1.jpg?w=1042&h=47

CRDB TABORA           Benki inayosikiliza Mteja CRDB Nao hawako Nyuma, Ofisi yao inatazamana na Uliokuwa uwanja wa Chipukizi. picha kwa hisani

https://uyui.files.wordpress.com/2013/05/kufungia-stori-1.jpg?w=1042&h=47

 rafiki guest house      Enzi Hizooooo!!!!! Nyumba ya kulala Wageni iitwayo Rafiki. ilikuwa maeneo ya Stendi ya zamani ya Mabasi

https://uyui.files.wordpress.com/2013/05/kufungia-stori-1.jpg?w=1042&h=47

Kuelekea Isevya                                                                                                                       Kuelekea Isevya, hapa ni maeneo ya stesheni

https://uyui.files.wordpress.com/2013/05/kufungia-stori-1.jpg?w=1042&h=47

Uyui: Simulizi za Abuu Omari kuhusu Tabora: Unamkumbuka Afande Zakaria?

Uyui: Simulizi za Abuu Omari kuhusu Tabora: Unamkumbuka Afande Zakaria?                                          

Historia yake kwa ufupi:

Prof OmariMimi naitwa Abbu Omar, NI mwanamuziki wa kitanzania niishie Tokyo, Japan,Nina asili yangu pia ya Tabora, Babu yangu mzaa mama ni Mmanyema bibi yangu mzaa mama ni Mnyamwezi, Baba yetu alitoka kwao kusini akiwa kijana na kuloea Tabora pia kumuoa mama yetu nasi tukazaliwa Tabora. Nilisoma shule ya msingi Town primary school ( Town school) kuanzia 1970, dada zangu walikuwa wakisoma Hr primary school enzi hizo (Siku hizi Abuu shule hiyo inaitwa Mwenge shule ya mazoezi). Nikasoma sekondari Songea boys high school.

 Maisha ya muziki:

 Maisha ya muziki niliyaanza na Uda Jazz, Dares Salaam, na kuhamia Nairobi Kenya 1981, huko nilipigia bendi maarufu ya Simba Wanyika kwa miaka 10. Mwakaa 1992 nikahamia Tokyo,Japan hadi sasa nipo huku.

 Wazee Maarufu wa Tabora anaowakumbuka:

Mimi ni mjukuu wa marehemu Mzee Swedi Juma wa Gongoni, mjini Tabora, Mzee huyu nae tunaweza kusema alikuwa maarufu maana alikuwa referee mkubwa Tabora miakaya 68, 69,hadi 70. Kwa wapenzi wa soka wa enzi hizo watamkumbuka, pia alikuwa referee mkali sana.(Marefa wengine maarufu Abuu enzi hizo pamoja na  Mzee Hamisi Msonga, Marehemu Mzee Bundala na Chambera). Watu wengine maarufu Tabora ambao walikuwa katika ukoo wetu ni marehemu mjomba wetu Athumani Tembo (Baba Nyota) yeye alikuwa mpiga solo wa Tabora Jazz kabla hata ya Shem Karenga kuja Tabora kutoka Kigoma.

 Mjomba wangu mwingine mzee Juma Swedi ndio alikuwa mmiliki wa ofisi au palipokuwa na Club ya Sungura sports club,fundi street, (Abuu Sungura ilishaifungaga Yanga bao Moja kwa bila 1-0 mwaka 1973 habari zake zikangazwa Dunia nzima kupitia BBC, DW ya Ujerumani na Radio Burundi

 Wazee wengine mashuhuri waliokuwa karibu na familia yetu ni

  1. Mzee Iddi Shaha,
  2. Mzee Iddi Pazi,
  3. Mafundi cherehani maarufu mtaa wa ngoma
  4. Mzee Hassan Famba na
  5. Mzee Hamisi Mbuli,

 Askari Polisi Zakaria

Askari polisi maarufu mjini Tabora enzi hizo Zakaria. Huyu alijulikana ukali wake hasa ktk mechi za mpira wa miguu. (Abuu huyu Afande Alikuwa anatembea na pingu, Rungu na filimbi kama afande shap- Mkama)  Mzee Shabani Kilima ,Askofu Kisanji wa Moravian church.Familia ya akina Rage,Mama Rage na tanzania hotel.

Mtaa wa Usagara

MImi nilizaliwa hospitali ya KItete na nilikulia kona ya   mtaa wa usagara na ngoma  street nyumba yetu kubwa ya mawe, ilitazamana na Amani hoteli,kulikuwa na vinyozi,baadae ikawa Ngorongoro hoteli,baadae ikauziwa mchaga akafanya baa, hapo ndipo kwetu.hizi habari sana sana ni za enzi za utoto wangu miaka ya 69 kuja mwisho wa 70’s ILa baadae tulihama na mzee kwa ajili ya yeye kupata transfer.Wajomba na bibi bado wako Tabora.

Uyui: Kutokana na umahiri wa Abuu aliweza kuitwa Prof Jn na wapenzi wa muziki

https://uyui.files.wordpress.com/2013/05/kufungia-stori-1.jpg

Uyui

A website about Uyui, Tabora heritages and the Wanyamwezi

Shahermohd's Blog

Just another WordPress.com site

WordPress.com

WordPress.com is the best place for your personal blog or business site.