Miaka 10 ya Soka la Tanzania Bila ya Said Mwamba Kizota (R.I.P- Said)

SAID NASSORO MWAMBA “KIZOTA”

Buriani Said Nassoro Mwamba “Kizota” mtambo wa magoli na Nyota ya Magharibi iliyozimika ghafla.

NI MIAKA 10 imepita sasa lakini nakumbuka ni kama tuliko lililotokea jana.  

ilikuwa tarehe 11 February, 2007 majira ya saa nne usiku nilipata ujumbe mfupi wa simu kutoka kwa Swedy Mwinyi wa Radio Tanzania, “.. salaam, Said Mwamba amefariki dunia kwa kugongwa na gari wakati anatoka Taifa!! Maiti ipo Mortuary Temeke..” Taarifa hii ya msiba, tena ya mtu unayemfahamu lazima imshitue mtu. Nilishituka sana baadaye nikamshukuru Mungu. Nilipigia simu mmoja wa Jamaa na rafiki wa karibu wa marehemu Said, Mchezaji wa zamani wa Simba na Yanga Kureish Ufunguo ambaye muda mfupi uliopita nilikuwa namtania kuhusu matokeo ya mechi ya Simba ya jana. Naye alishituka sana, masikini, naye  hakuwa na taarifa akaniambia labda tumuulize Isack Gamba wa Radio One, nilipompigia akasema ni kweli!!. Ndivyo yalivyo maisha ya mwanadamu hapa duniani, kama Ua huchanua na kusinyaa.

Kwa mtu yeyote aliyemfahamu marehemu Said, atakiri na kukubaliana nami kuwa Taifa limepoteza mmoja wa mashujaa wake aliyelipigania Taifa lake katika medani ya Soka enzi za uhai wake. Alikuwa na kipaji cha ajabu katika soka na aliufanya mpira jinsi alivyotaka yeye.

Marehemu Said Mwamba alizaliwa na kukulia mjini Tabora kabla ya kuja Dar es Salam miaka ya 1980 katikati ambapo baadaye alijiunga na  Dar es Salaam Youngs Africa (YANGA). Ameifanyia mengi Klabu hii ya Jangwani ambayo licha ya kuwa mchezaji alikuwa ni mdau wake mkubwa.

Kwa kipindi cha takribani miongo mitatu iliyopita Tabora ilikuwa ni mji uliotoa wachazaji wengi wenye vipaji tangia enzi za Gosaji Cup miaka ya 1960 kama Yunge mwana Sali, Hasan Rajab, Mzee kitenge na wengineo. Miaka ya 1970 kukawa na timu imara kama Sungura, Coastal, baadaye Tumbaku, Tindo, na Vita iliyokuwa Timu ya Jeshi enzi za Meja Jenerali mstaafu Mayunga alipokuwa mkuu wa Brigedi ya Magharibi.

Wakati marehemu Said anaanza kucheza mpira yeye na ndugu zake kina Rajabu na Ally Mwamba, kina Ufunguo na Abas Mchemba tayari Tabora imelishawahi kutoa wachezaji wenye vipaji walioliwakilisha Taifa kama kina Amasha, Athumani Maulidi-Big man, Hamis Kinye,  marehemu Athumani Mambosasa, Rajab Risasi, Abdallah Mwinyimkuu pele ambao walimsawishi marehemu Said kuongeza bidii.

walikuwepo pia watu waliosomea shule za Tabora kama Daudi Salum Bruce Lee na marehemu Ibrahim Marekano Regan ambao walipata mafanikio makubwa na kuchezea timu ya wekundu wa Msimbazi Simba ziku za nyuma. Tabora ilikuwa na kituo cha kuibua vipaji vya watoto wadogo cha kanisa katoliki Tabora kilichokuwa chini ya ulezi wa father Damiano cha Chipukizi.

Ndani ya uwanja marehemu Said alikuwa na uwezo wa kucheza karibu namba zote. Alipotoka Tabora na kujiunga Yanga alikuwa anacheza nafasi ya kiungo mkabaji. Baadaye waalimu kama sikosei ni marehemu Tarzan alimbadili na kumfanya acheze kama mshambuliaji wa kati.  Kuna wakati nilimuuliza sababu gani ilimfanya aende Simba kabla ya kuridi tena Yanga, akatabasamu na kuniambia kuwa mpira una mambo mengi.

Said alikuwa na uwezo mkubwa wa kupiga chenga tena za maudhi halafu anaukanyaga mpira na kuwaangalia wachezaji wa timu pinzani kama anayeuliza maswali? Kutokana na uwezo wake wa kumiliki mpira alifananishwa na jinsi marehemu baba wa Taifa alivyokuwa anaendesha vikao vya Chama kule kizota alipokuwa akiuliza maswali? Huku wajumbe wakisema hakunaa.

Wapenzi wa kandanda watakubaliana nami kuwa marehemu Said alikuwa na kipaji kikubwa. Mwaka 1993 alikuwa ni miongoni mwa wachezaji walioiwezesha  Yanga kuutwaa Ubingwa wa Afrika ya Mashariki. Enzi hizo walikuwapo kina keneth Mkapa, Nemes, Mohammed Hussein Mmachinga, Abubakar Salum, Mwanamtwa Kihwelo, Zamoyoni Mogella, Edbily Lunyamila, marehemu Steven Mussa, Gagarino, marehemu Method Mogella na marehemu Riffat Said.

Marehemu Said Mwamba, mbali ya mafanikio aliyopata ndani ya uwanja, nje ya uwanja aliuweka kando u-super star wake, hakuwa mtu wa kujidai, alikuwa hawezi kumpita mtu aliyemfahamu bila kusimama na kumsalimia. Kuna habari ambazo sikuwahi kumuuliza marehemu said kama kweli alishawahi kuukataa uraia wa moja ya nchi za kiarabu (Abudhabi) ili aendelee kuchezea Yanga.

Wapo wachezaji ambao hata wenzao wanawakubali. Said ni mmoja wa wachezaji ambao hata wa Timu ya Taifa mwaka 2000 wakati tunajiaanda kucheza na Ghana wachezaji wenzake walimtaka kocha mkuu wa timu ya Taifa Mjerumani Bukhard Pape awaite kikosini Kizota na Masatu ili achwe huru  kama wanamfaa

Nilipomuuliza kama kuna Timu nyingine aliyowahi kuipenda kama Yanga, marehemu Said alisema kuwa alikuwa anapenda sana uchezaji wa Timu ya Pamba wana kawe kamo enzi hizo ilipokuwa kwenye kiwango.

Taifa na wapenzi wa mpira hasa wa Yanga wamepata msiba mkubwa na vivyo hivyo kwa hata kwa wapenzi na wanachama wa Simba ambao marehemu alipata kuchezea.  Kwa hali yeyote iwayo msiba huu ni mkubwa sana Tabora kwa sababu mji huo umepoteza mmoja wa watoto wake wenye vipaji vikubwa iliyopata kuwazaa. Wapo wachezaji wengi lakini alikuwapo Said Mwamba kizota mmoja na pengine itachukuwa miongo kadhaa kumpata wa mithili yake.

Wapo wachezaji wengi lakini alikuwepo Said Mwamba Kizoto Mmoja tu Tanzania.Buriani Said Mwamba kizota umetangulia kule ambako sisi tuliobaki tutakufuta. Wote tumetoka kwa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.

Advertisements

Uyui: Simba yalala kwa Mtibwa

Simba lost to Mtibwa… but shouldn’t lose a lesson.

Washakibiki wa Simba wawe na subira timu yao inapoteleza

Simba yalala kwa Mtibwa

Simba Sports Club, lost 0-2 to Mtibwa Sugar of Morogoro. Winning and losing a game or ending up in a deadlock in a football game is what football is all about, after all, thats what is expected. We are tempted to come up with this story simply because Simba was the only unbeaten team in the Vodacom Premier League, before tamed by Mtibwa today. Before the game, Simba had a series of deadlock games. In Tanzanian soccer politics someone will have to be sacrificed. It happened to Yanga and Azam who sacked their Coaches after being defeated in crucial matches, hope it will not happen to Simba’s coach. Once beaten, twice shy. Simba has already lost a game it should not further lose the lesson from its recent trend. They need to be sober and analytical rather than jumping to a conclusions which often lack basis

Simba imefungwa na Mtibwa sawaaaa hatuna tatizo…. tatizo ni kuwa wamejifunza nini???.

Katika Ligi Kuu inayoendelea hapa Bongo, hatimaye Timu pekee iliyosalia bila kufungwa ya Wekundi wa Msimbazi, hatimaye imesalimu amri kwa wakata miwa wa Mtibwa kwa kufungwa magoli mawili kwa bila (2-0). Kwenye mpira matokeo yoyote hutegemewa na pengine hiyo sio sababu iliyotufanya tuandike habari hii. Kilichotufanya kuandika ni namna timu kubwa kama Simba, Yanga au Mtibwa zinapofungwa tu hasa mechi muhimu hutafuta njia rahisi ya ufumbuzi. Mara nyingi huishia kufukuza makocha. Hii imeshatokea kwa Yanga na Azam. Sidhani kama itatokea kwa Simba. Simba wanao wajibu wa kutulia zaidi na kutafuta chanzo cha timu yao kuwa na sare za mfululizo kabla ya kufungwa.

Simba yalala.

magangaferuzi@gmail.com


Uyui: Yanga na Simba kutoka Tabora na Morogoro Enzi hizo ( Simba and Young African Giant footballers from Tabora and Morogoro)

Mchango wa Mikoa ya Tabora na Morogoro katika soka la nchi hii ni mkubwa sana. Hebu angalia safu hizi kutoka Tabora na Morogoro. Hawa wamepata kusoma, kucheza au kufanya kazi katika mikoa hii miwili. Tabora na Morogoro inaunganishwa na vitu vikubwa viwili cha kwanza ni watani na pili ni kile kiwanda cha Tumbaku. Tabora ililima, Morogoro ikawa na kiwanda cha Tobacco processing na tatu Wanyamwezi wakipita na Treni kutoka Tabora lazima wapite ya Morogoro hapo kabla ya kuingia Dar. Morogoro kuna Bahari ya Mindu(Bwawa), Tabora kuna Bahari ya Igombe (Bwawa)

TABORA -SIMBA

Marehemu Mambosasa (jezi ya njano) na Mwinyimkuu(waliochuchumaa wa pili kutoka kushoto) wote walikuwa vijana kutoka Tabora.

Wachezaji hawa ama wamezaliwa tabora au wamesomea Tabora au wamepata kucheza mpira Tabora kabla ya kuingia Timu za Simba na Yanga ambapo wengine walifanikiwa kuwa viongozi (Mfano Mwenyekiti wa Sasa wa Simba Alhaji Ismael Aden Rage). picha na blog ya michuzi
1.Athumani Mambosasa R.I.P
2.Mzee Hamis Fikirini (R.I.P)
3.Athumani Maulidi (Big Man) R.I.P
4.Mrisho Moshi
5.Haruna Moshi (Boban)
6. Abdallah Mwinyimkuu (Pele)
7.Ismael Aden Rage (Mwenyekiti wa Sasa wa Simba)
8.Kureish Ufunguo
9.Mrage Kabange (amecheza Tabora)
10.Daudi Salum “Bruce Lee”(Tabora Boys)kutoka Morogoro
11.Ibrahim Marekano (Regan)
12.Zubeir Rehani Malingo (Bwana Jela)
13. Ismael Mwarabu
14 Mtemi Ramadhani (amepata kucheza Tabora)
15 Renatus Njohole (alichezea Mirambo kabla ya kwenda Simba)

Marehemu Said Mwamba Kizota

TABORA-YANGA
1.Hamis Kinye
2.Ahmed Abdul Thabit (Amasha)- Uyui baadaye Kazima Sekondari
3.Shaban Katwila (Uyui Secondary)
4.Adam Katwila
5.Mikidadi Jumanne (Bubu wa Yanga)
6.Iddi Moshi (Mnyamwezi)
7.Said Nassoro Mwamba (Kizota)
8 Stephen Mataluma
9. Jobe Ayubu (alichezea mirambo)
Tabora imekuwa na wachezaji ambao ni Hazina kubwa kama Abbas Mchemba(African Sports- alishawaliza sana Simba mpaka wakasingizia mvua), Dickson Kanumba (Reli), Rajab Risasi-Jiji (Pamba ya Mwanza)

KUTOKA MKOA WA MOROGORO

MOROGORO-YANGA

charles Boniface alipata kucheza Morogoro

1. Marehemu Gibson Sembuli
2. Jellah Mtagwa
3. Abrahman Juma
4. Chalres Boniface Mkwasa (Master)
5. Juma Matokeo
6. Hamis Gaga (Yanga/Simba)
7. Omar Hussein (Keegan)
8. Juma Shaban

MOROGORO-SIMBA

zamoyoni. picha hisani ya michuzi blogspot

1. Zamoyoni Mogella
2. Hassan Mlapakolo
3. Aluu Ally
4.Omari Chogo (Choggo Chemba)
5. Malota Soma
6. Adam Sabu
Wamekuwepo wachezaji kama Idris Ngulungu, Manga na Shiwa Lyambiko ambao walikuwa na uwezo mkubwa wa kuchezea Simba au Yanga lakini walibakia kuchezea Timu za Morogoro.

SIMBA AND YANGA LEGENDS FROM TABORA AND MOROGORO REGIONS
This is a collection of big names from Tabora and Morogoro Regions (lukwangule) who played for Tanzania great team i.e Simba and Yanga. The legends had a historical success in their career and left foot prints which we all cherish when talking Tanzanian footbal. We shall appreciate to have more updates on the list or corrections if any so that the contributions made by the players, some from Uyui Secondary, Kazima Secondary and Tabora Boys are not skipped in the historical books of football for Tabora as well as Morogor and Other sister Region like Kigoma where the Manara Family (Kitwana, Sunday, Kassim) are comming from. Kaseja, Mavumbi Omari Hamza Maneno, Lunyamila and others. Let turn back and explore more from these regions so that our soccer standards rises again.

Posted in Soka. Tags: , , , . 4 Comments »
Uyui

A website about Uyui, Tabora heritages and the Wanyamwezi

Shahermohd's Blog

Just another WordPress.com site

WordPress.com

WordPress.com is the best place for your personal blog or business site.