All the best “the might” Serengeti Boys

U-17 National Team, Serengeti Boys

U-17 National Team, Serengeti Boys

TIMU ya Taifa ya vijana wa umri chini ya miaka 17 Serengeti Boys, kesho inajitupa dimbani kuchuana na wenzao wa Congo Brazaville katika mechi ya kuwania kufuzu michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mwakani.

Sisi wa Uyui tunaitakia kila la heri timu yetu hii ya vijana. Hii pia inatukumbusha enzi ya timu ya Chipukizi pale Tabora ambapo Buruda Damiano wa Mihayo alikuwa akichuwa muda mwingi kushughulika na soka la vijana hasa chipukizi na matokeo yake alitoa wachezaji bora na imara walioliwakilisha taifa. Kila la heri Serngeti boys. Vyovyote iwavyo ninyi ni mashujaa wa taifa letu. kitu cha msingi ni kuishangilia timu yetu mwanzo mwisho na kuhakikisha tunasonga mbele. Kingine ni kuhakikisha kuwa timu hii inadumu. Tunajua hili lina gharama zake, tunajua pia vipo vilabu vitataka kuwavuta vijana hawa ili wasajiliwe na timu zao. ifike mahali tujifunze na tupige hatua kama hii tuliyoanza sasa.
Kufungia Stori 1

Uyui

A website about Uyui, Tabora heritages and the Wanyamwezi

Shahermohd's Blog

Just another WordPress.com site

WordPress.com

WordPress.com is the best place for your personal blog or business site.