Icons and Celebrities of Tabora


 

SAID NASSORO MWAMBA “KIZOTA”

 

 

Buriani Said Nassoro Mwamba “Kizota” mtambo wa magoli na Nyota ya Magharibi iliyozimika ghafla.

 

 

Jana majira ya saa nne usiku nilipata ujumbe mfupi wa simu kutoka kwa Swedy Mwinyi wa Radio Tanzania, “.. salaam, Said Mwamba amefariki dunia kwa kugongwa na gari wakati anatoka Taifa!! Maiti ipo Mortuary Temeke..” Taarifa hii ya msiba, tena ya mtu unayemfahamu lazima imshitue mtu. Nilishituka sana baadaye nikamshukuru Mungu.

 

Nilipigia simu mmoja wa Jamaa na rafiki wa karibu wa marehemu Said, Mchezaji wa zamani wa Simba na Yanga Kureish Ufunguo ambaye muda mfupi uliopita nilikuwa namtania kuhusu matokeo ya mechi ya Simba ya jana. Naye alishituka sana, masikini, naye  hakuwa na taarifa akaniambia labda tumuulize Isack Gamba wa Radio One, nilipompigia akasema ni kweli!!. Ndivyo yalivyo maisha ya mwanadamu hapa duniani, kama Ua huchanua na kusinyaa.

 

Kwa mtu yeyote aliyemfahamu marehemu Said, atakiri na kukubaliana nami kuwa Taifa limepoteza mmoja wa mashujaa wake aliyelipigania Taifa lake katika medani ya Soka enzi za uhai wake. Alikuwa na kipaji cha ajabu katika soka na aliufanya mpira jinsi alivyotaka yeye.

 

Marehemu Said Mwamba alizaliwa na kukulia mjini Tabora kabla ya kuja Dar es Salam miaka ya 1980 katikati ambapo baadaye alijiunga na  Dar es Salaam Youngs Africa (YANGA). Ameifanyia mengi Klabu hii ya Jangwani ambayo licha ya kuwa mchezaji alikuwa ni mdau wake mkubwa.

 

Kwa kipindi cha takribani miongo mitatu iliyopita Tabora ilikuwa ni mji uliotoa wachazaji wengi wenye vipaji tangia enzi za Gosaji Cup miaka ya 1960 kama Yunge mwana Sali, Hasan Rajab, Mzee kitenge na wengineo. Miaka ya 1970 kukawa na timu imara kama Sungura, Coastal, baadaye Tumbaku, Tindo, na Vita iliyokuwa Timu ya Jeshi enzi za Meja Jenerali mstaafu Mayunga alipokuwa mkuu wa Brigedi ya Magharibi.

 

Wakati marehemu Said anaanza kucheza mpira yeye na ndugu zake kina Rajabu na Ally Mwamba, kina Ufunguo na Abas Mchemba tayari Tabora imelishawahi kutoa wachezaji wenye vipaji walioliwakilisha Taifa kama kina Amasha, Athumani Maulidi-Big man, Hamis Kinye,  marehemu Athumani Mambosasa, Rajab Risasi, Abdallah Mwinyimkuu pele ambao walimsawishi marehemu Said kuongeza bidii.

 

walikuwepo pia watu waliosomea shule za Tabora kama Daudi Salum Bruce Lee na marehemu Ibrahim Marekano Regan ambao walipata mafanikio makubwa na kuchezea timu ya wekundu wa Msimbazi Simba ziku za nyuma. Tabora ilikuwa na kituo cha kuibua vipaji vya watoto wadogo cha kanisa katoliki Tabora kilichokuwa chini ya ulezi wa father Damiano cha Chipukizi.

 

Ndani ya uwanja marehemu Said alikuwa na uwezo wa kucheza karibu namba zote. Alipotoka Tabora na kujiunga Yanga alikuwa anacheza nafasi ya kiungo mkabaji. Baadaye waalimu kama sikosei ni marehemu Tarzan alimbadili na kumfanya acheze kama mshambuliaji wa kati.  Kuna wakati nilimuuliza sababu gani ilimfanya aende Simba kabla ya kuridi tena Yanga, akatabasamu na kuniambia kuwa mpira una mambo mengi.

 

Said alikuwa na uwezo mkubwa wa kupiga chenga tena za maudhi halafu anaukanyaga mpira na kuwaangalia wachezaji wa timu pinzani kama anayeuliza maswali? Kutokana na uwezo wake wa kumiliki mpira alifananishwa na jinsi marehemu baba wa Taifa alivyokuwa anaendesha vikao vya Chama kule kizota alipokuwa akiuliza maswali? Huku wajumbe wakisema hakunaa.

 

Wapenzi wa kandanda watakubaliana nami kuwa marehemu Said alikuwa na kipaji kikubwa. Mwaka 1993 alikuwa ni miongoni mwa wachezaji walioiwezesha  Yanga kuutwaa Ubingwa wa Afrika ya Mashariki. Enzi hizo walikuwapo kina keneth Mkapa, Nemes, Mohammed Hussein Mmachinga, Abubakar Salum, Mwanamtwa Kihwelo, Zamoyoni Mogella, Edbily Lunyamila, marehemu Steven Mussa, Gagarino, marehemu Method Mogella na marehemu Riffat Said.

 

Marehemu Said Mwamba, mbali ya mafanikio aliyopata ndani ya uwanja, nje ya uwanja aliuweka kando u-super star wake, hakuwa mtu wa kujidai, alikuwa hawezi kumpita mtu aliyemfahamu bila kusimama na kumsalimia. Kuna habari ambazo sikuwahi kumuuliza marehemu said kama kweli alishawahi kuukataa uraia wa moja ya nchi za kiarabu (Abudhabi) ili aendelee kuchezea Yanga.

 

Wapo wachezaji ambao hata wenzao wanawakubali. Said ni mmoja wa wachezaji ambao hata wa Timu ya Taifa mwaka 2000 wakati tunajiaanda kucheza na Ghana wachezaji wenzake walimtaka kocha mkuu wa timu ya Taifa Mjerumani Bukhard Pape awaite kikosini Kizota na Masatu ili achwe huru  kama wanamfaa

 

Nilipomuuliza kama kuna Timu nyingine aliyowahi kuipenda kama Yanga, marehemu Said alisema kuwa alikuwa anapenda sana uchezaji wa Timu ya Pamba wana kawe kamo enzi hizo ilipokuwa kwenye kiwango.

 

Taifa na wapenzi wa mpira hasa wa Yanga wamepata msiba mkubwa na vivyo hivyo kwa hata kwa wapenzi na wanachama wa Simba ambao marehemu alipata kuchezea.  Kwa hali yeyote iwayo msiba huu ni mkubwa sana Tabora kwa sababu mji huo umepoteza mmoja wa watoto wake wenye vipaji vikubwa iliyopata kuwazaa. Wapo wachezaji wengi lakini alikuwapo Said Mwamba kizota mmoja na pengine itachukuwa miongo kadhaa kumpata wa mithili yake.

 

Buriani Said Mwamba kizota umetangulia kule ambako sisi tuliobaki tutakufuta. Wote tumetoka kwa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.

SAID MWAMBA IS NO MORE

 

FROM ippmedia.com 2007-02-13 09:26:57
By Guardian Reporter

 

Former Taifa Stars and Yanga player Said Mwamba `Kizota` has died. Kizota died on Sunday after being knocked down by an identified car at Tazara/Mandela junction when he was crossing the road.

The player was on his way back home from the National Stadium after watching the Confederation Cup, return leg match between Simba and Textile du Mpungue.
The Mozambican side eliminated Simba on a 5-3 aggregate.

According to one witness, Kizota died at 1 pm at the Temeke Hospital where Good Samaritans had rushed him for treatment after a saloon car which had knocked him down disappeared.

“It is very sad to hear that Kizota has died. We were together with him at the stadium yesterday when Simba were playing Textile du Pungue,“ said coach Syllersaid Mziray who once trained him during his heyday at Yanga.
The body of the deceased was expected to be buried yesterday in Dar es Salaam.

Kizota was an all-rounder as he could play as midfielder, defender and attacker.

He helped Yanga lift the East and Central Club Championship when he co-ordinated well with players like Edibily Lunyamila, Mohamed Hussein and Sekilojo Chambua, to mention but a few.

The Football Association of Tanzania (FAT), now Tanzania Football Federation (TFF), voted him the best footballer of the year in 1993.

Before joining Yanga, Kizota had played for Tindo of Tabora and Pan African.
May God rest his soul in eternal life.

Advertisements

11 Responses to “Icons and Celebrities of Tabora”

 1. MNUBI MIKIDADI BAGUMA Says:

  KIZOTA hakamiliki bila kuitaja timu iliyomuibua ya POSTA TABORA

 2. Mariam Masanja Says:

  Ina Lillahi wa ina illaihi rajjiun. RIP mwana kwetu

 3. Diedra Aroyo Says:

  many thanks, it’s simply accessible and has countless great ideas and tips. the primary of my 2 favorite options are the pages where they’ll begin with an item or a handful of things that function inspiration for your space, after which detail how the house owner used those things to form a novel and well-styled house.

 4. ERASMO MULLICK Says:

  Good article,I like it very much!

 5. JB Says:

  NIMEKUA NIKIMUONA ANACHEZA UWANJA WA VITE NA POSTER. R I P MTT WA UKOO WA WALIMU. MTT WA MBUGANI MTABORA HALISI. NIKIWA KAMA MTT WA WATO 100 MASHUGHULI TBR MZEE KASSONGO NAKUBALIANA NA SAIDI MWAMBA KUWA KTK ORODHA HIYO!

 6. http://www.youi.com.au/ Says:

  I like material like this. This is a great article and I really enjoyed reading it. You have an original style that makes your ideas stand out from other writers.

 7. Myong Kuney Says:

  I was suggested this website by my cousin. I am not sure whether this post is written by him as nobody else know such detailed about my trouble. You’re incredible! Thanks!

 8. Indonesia Says:

  You have managed to write an interesting and unique article that kindled my interest. There are many solid points that make the reader think. I can think of nothing better than an original thought-provoking article.

 9. bekar bayan arkada Says:

  This article is top notch. I salute you on your use of words and research on this topic. Please do not stop making these. They are high quality and some of the best I’ve seen.

 10. Lisas site Says:

  Only an open-minded person could write this kind of content. I agree with your points and I really enjoyed this article a lot. Great article!

 11. Fletcher Deflorio Says:

  So little done, so much to do.


Leave a Reply (Please be decent) Acha ujumbe wako hapa (kuwa mstaarabu)

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Uyui

A website about Uyui, Tabora heritages and the Wanyamwezi

Shahermohd's Blog

Just another WordPress.com site

WordPress.com

WordPress.com is the best place for your personal blog or business site.

%d bloggers like this: